RAIS KIKWETE AKITAKA CHUO CHA TAIFA CHA ULINZI TANZANIA KUWEKEZA KATIKA TAFITI ZA HALI YA JUU


Rais Jakaya Kikwete amekitaka chuo cha taifa cha ulinzi Tanzania-NDC- kuwekeza katika tafiti za hali ya juu zitakazosaidia kutatua matatizo ya nchi za Afrika husasani katika changamoto zinazotokana na maswala ya ulinzi.


Akitunuku vyeti kwa wahitimu 31 wa mafunzo ya usalama na ya kimakakati, rais Kiwete amesema chuo cha taifa cha ulinzi Tanzania kinapaswa kuwa kitovu cha fikra katika maswala yanayohusu ulinzi kwa kufanya tafiti za hali ya juu zitakazo weza kukitambulisha ndani na nchi ya Tanzania.

Kwa upande wake mkuu wa chuo cha taifa cha ulinzi Meja Jenerali Gaudence Milanzi amesema lengo la chuo hicho kuwa ni kuwa katika kiwango kinachokubalika kimataifa na kuwa kituo muhimu katika maendeleo ya ulinzi nchni ambapo amesema mpaka sasa tayari kinatoa mafunzo kwa viongozi katika sekta ya ulizni, taasisi za umma na nchi marafiki.

Zaidi ya wahitimu 31, wakiwemo watanzania 21 na wengine kutoka nchni za Botswana, Kenya, Malawi, Nigeria, Zambia, Zimbabwe na Namibia wametunukiwa vyeti na rais Jakaya Kikwete baada ya kupata mafunzo yakiwemo ya ulinzi kwa zaidi ya wiki 47.
Via>>ITV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post