News Alert! HUYU NDIYO MGOMBEA WA UBUNGE SHINYANGA MJINI KUPITIA CHADEMA 2015!!


Habari tulizozinyaka hivi punde kutoka kwenye mkutano wa uchaguzi wa kutafuta wagombea wa ubunge na viti maalumu Chadema uliokuwa unafanyika katika ukumbi wa Ibanza Hotel mjini Shinyanga leo ni kwamba ndugu Paschal Patrobas Katambi(Mzimu wa Shelembi),ambaye ni mwenyekiti wa Baraza la Vijana Chama Cha Maendeleo (Chadema) Taifa,amechaguliwa na wanachama wa chama hicho kugombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini kupitia Chadema/Ukawa katika uchaguzi mkuu ujao.

Watia nia ya ubunge walikuwa 11 ingawa Katambi alikuwa anachuana vikali na Rachel Mashishanga aliyepata kura 53,na Francis Kasili aliyepata kura 63 wakati yeye (Katambi) akipata kura 78.

Kwa matokeo hayo,Patrobas Katambi ambaye amekuwa akijiita Mzimu wa Shelembi ndiyo atasimama kugombea ubunge jimbo la Shinyanga Mjini kupitia Chadema/Ukawa katika uchaguzi mkuu ujao.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post