NAHAMA,SIHAMI YA MADIWANI YAWAVURUGA WANANCHI WA MONDULI," WAWATAKA WANASIASA WAACHE UJINGA"



Hali ya kisiasa kati ya CCM na Chadema katika wilaya ya Monduli imegubikwa na sinto fahamu na kuwachanganya wananchi wasijue pakuelekea baada ya madiwani 10 kati ya 18 wa CCM waliodaiwa kuhamia Chadema kusema bado wapo CCM na tayari wameshachukua na kurudisha fomu za kutetea nafasi zao huku wananchi wakiwataka wanasiasa waache kuwachanganya kwa kuwafanya wajinga.

Baadhi ya madiwani walio daiwa kuondoka CCM wamesema kauli hizo hazikuwa za kweli kwakuwa baadhi yao walikuwa hawaja hafiki mpango huo na kwamba wanaendelea kuheshimu taratibu za chama chao huku wakidai wanatetea nafasi zao kupitia CCM.

ITV ilimtafuta mwenyekiti wa madiwani waliohama aliyekuwa diwani kata ya Lepurko Julias Kalanga ambaye amesema kilichopo ni baadhi ya watu kukosa kujiamini katika jambo wanalolifanya na kwamba wanataka kuficha moto usiofichika na kuwachanganya wananchi lakini siku ikifika ukweli utajulikana .

Katibu wa CCM mkoa wa Arusha Alphonce Kinamhala akithibisha madiwani hao kuchukua fomu za kugombea kupitia CCM na kwamba hizo zilkuwa mbinu za watu kuichafua CCM.

Wakazi wa Monduli ambao wameonesha kusikitishwa na hatua ya wanasiasa kutokuwa wakweli na kuwataka wasiwachanganye kwani wananchi wa sasa siyo wa miaka ya nyuma pamoja na yote lakini watafanya maamuzi yenye maslahi kwao na siyo vinginevyo.

Via>>ITV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post