MTANGAZAJI MAARUFU WA ITV GODWIN GONDWE ACHUKUA FOMU KUGOMBEA UBUNGE JIMBO LA ILEMELA


October 25 2015 ni siku ya Uchaguzi Mkuu ambapo Watanzania watachagua Rais, Wabunge na Madiwani.. sababu hiyo pekeyake inatosha kutufanya tusikwepe kabisa kukutana na stori za kisiasa Tanzania !!

Idadi ya Wanahabari waliotangaza Kugombea Ubunge kwenye Majimbo mbalimbali Tanzania imezidi kuongezeka, tumesikia kuhusu wengi ikiwemo mmoja ya Wanahabari wakongwe Tanzania, Godwin Gondwe ambaye ametangaza kugombea Ubunge wa Jimbo la Ilemela Mwanza.

Godwin Gondwe anagombea Jimbo hilo na Sera yake ni hii >>>> ‘MABADILIKO NI SASA, KURA YAKO INA THAMANI KWA MAENDELEO YA ILEMELA‘
Hapa ninayo picha inayothibitisha kwamba tayari Godwin Gondwe amechukua fomu ya Kugombea Ubunge wa Jimbo hilo Mwanza.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post