MBUNGE JAMES LEMBELI AFUNIKA MBAYA KWENYE MKUTANO WA CHADEMA MJINI KAHAMA,ABEBWA KWENYE KITI


Mheshimiwa James Lembeli akiwa amebebwa

Maelfu ya wakazi wa mji wa Kahama wamejitokeza kumpokea aliyekuwa mbunge wa Kahama James Lembeli huku mbunge huyo akiwataka wananchi kuunga mkono safari yake ya kupiga vita Rushwa matumizi mabaya ya mali za umma na rasilimali za taifa ili kuwezesha ukombozi wa watanzania katika kupambana na umasikini.


Akizunguza na umati wa watu waliompokea kwa shangwe na bashasha za hali ya juu James Lembeli huku akinuukuu maandiko matakatifu ya bibila amesema maamuzi yake ameyafanya baada ya kuzingatia mambo muhimu katika ukombozi wa watanzania ambayo asingeweza kuyatimiza kama angeendelea kuwa katika familia ya CCM iliy jaa wasaliti waliosababisha yeye kuondoka.

Naye mwenyekiti wa taifa wa baraza la vijana wa Chadema Patrobas Katambi amesema vijana wa Tanzania wamekata tamaa ya kuishi maisha mazuri kwa kuwa matatizo yamekuwa sugu katika kila sekta ukianzia elimu afya na mengineyo kwani hata fedha za serikali zimekuwa ni za mafisadi wachache huku wananchi wakiendelea kuteseka.

Akihitimisha kauli za Chadema kwa mbunge wa Nyamagana Ezekia Eenje amesema Chadema imefanya kazi kubwa katika kuikomboa Tanzania na sasa umefika wakati wa wananchi kufanya maamuzi yatakayohitimisha juhudi za Chadema katika ukombozi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post