ANGALIA PICHA_ BARAZA LA MADIWANI MANISPAA YA SHINYANGA LAVUNJWA,MKUU WA MKOA AWAONYA MADIWANI WATALII




Hapa ni katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga mkoani Shinyanga ambako leo kumefanyika Kikao cha Kuvunja baraza la Madiwani wa manispaa ya Shinyanga kwa ajili ya kupisha/kujiandaa na uchaguzi mkuu ujao wa madiwani,ubunge na rais.Mgeni rasmi alikuwa mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga.Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog Shinyanga



Awali naibu meya wa manispaa ya Shinyanga David Nkulila akifungua kikao cha madiwani wa manispaa hiyo,ambapo pamoja na mambo mengine alitumia fursa hiyo kuwashukuru madiwani na watendaji wa serikali kushirikiana kwa pamoja katika kuwaletea maendeleo wananchi na kuwatakia kila kheri wataobahatika kurudi kwenye baraza hilo.
Madiwani wakiwa ukumbini

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiingia ukumbini na mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga

Madiwani wakiwa ukumbini


Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza katika kikao hicho ambapo aliwataka madiwani hao kuendeleza undugu wao ikiwemo kusameheana kama walikwazana katika kipindi cha miaka mitano cha uongozi wao ili waweze kuanza upya katika kipindi kijacho.


Kaimu mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga Pudensiana Kihawa akizungumza katika baraza hilo la madiwani,ambapo pamoja na mambo mengine aliwashuru watalaamu wa manispaa hiyo kwa kushirikiana kwa pamoja kuifanya manispaa hiyo ipate hati safi kwa miaka mitano mfululizo


Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga akitoa hotuba yake wakati wa kikao hicho cha baraza la Madiwani ambapo alisema katika kipindi cha miaka mitano ya baraza hilo,kumekuwa na uhusiano mbovu kati ya watendaji wa serikali na madiwani hali iliyosababisha manispaa hiyo kufanya vibaya katika utekelezaji wa ujenzi wa maabara za shule za sekondari hali iliyofanya manispaa hiyo iwe ya pili kutoka mwisho kati ya halmashauri sita za mkoa huo.

Madiwani wakiwa ukumbini



Rufunga alisema katika kipindi cha miaka mitano ,kulikuwa na hali ya dharau na hali ya madiwani kutotii maagizo yanayotoka serikalini,kitendo kilichosababisha baadhi ya madiwani kuzuia wananchi wasichangie shughuli za maendeleo hususani katika ujenzi wa maabara katika shule za sekondari.



Rufunga alisema katika kutekeleza agizo la rais la ujenzi wa maabara manispaa ya Shinyanga,imefanya vibaya imetekeleza kwa asilimia 40 tu na halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Vijijini asilimia 35,Kishapu asilimia 90,wakati halmashauri za Ushetu,Msalala na Kahama Mji wakiwa wametekeleza kwa asilimia 100.



Akizungumza katika kikao cha madiwani wa manispaa ya Shinyanga Rufunga aliwataka madiwani ambao walitumia nafasi ya udiwani kufanya utalii badala ya kuwaletea maendeleo wananchi waachane na nafasi hiyo katika uchaguzi ujao kwani wananchi wanahitaji viongozi wachapakazi badala ya viongozi watalii.




Aliyekuwa mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga Festo Kang’ombe ambaye sasa ni katibu tawala wa mkoa wa Singida akiwaaga watendaji na madiwani wa manispaa ya Shinyanga.



Mstahiki meya wa manispaa ya Shinyanga Gulam Hafidh Mukadam akizungumza wakati wa kuvunja baraza la madiwani wa manispaa hiyo.Pamoja na mambo mengine aliwapongeza madiwani na watendaji wa serikali kwa ushirikiano wao mzuri katika kutekeleza mambo mbalimbali ya kimaendeleo hali iliyosababisha manispaa hiyo ipate hati safi kwa miaka mitano mfululizo.


Mstahiki meya wa manispaa ya Shinyanga Gulam Hafidh Mukadam akivunja baraza la madiwani wa manispaa hiyo kwa ajili ya kujiandaa na uchaguzi mkuu ujao

Madiwani wakapiga picha ya kumbukumbu na mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga,huku wengine wakiwaza Sijui Ntarudi tena!!



Picha za kumbukumbu zikaendelea kupigwa....



Picha ya kumbukumbu



Picha ya pamoja,Madiwani na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Shinyanga



Picha ya pamoja,madiwani na watumishi wa manispaa ya Shinyanga



Wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya Shinyanga wakiwa ukumbini


Picha zote na Kadama Malunde- Malunde1 blog Shinyanga

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post