ANGALIA HAPA JINSI RAIS OBAMA ALIVYOTUA MJINI NAIROBI
Rais Barack Obama

Akisalimiana na ndugu zakeNdege ya Obama katika Uwanja wa JKIA


Wakenya wakifuatilia ziara ya Obama kwenye runinga


Rais Barrack Obama wa Marekani, tayari amewasili mjini Nairobi.

Ndege iliyombeba rais obama ilitua katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta muda mfupi baada ya saa mbili za usiku.

Alipowasili Rais Obama amelakiwa na mwenyeji wake Rais Uhuru Kenyatta.

mwendo wa saa mbili na robo rais Obama alitua ndege yake.

Alipowasili alizungumza kwa muda mfupi na mwenyeji wake rais Kenyatta na kisha kutia saini kitabu cha wageni kabla ya kuondoka.

Obama sasa ameandikisha historia ya kuwa rais wa kwanza wa Marekani, kuzuru Kenya akiwa ofisini.

Obama anatarajiwa kufungua mkutano wa sita wa kimataifa kuhusu ujasiri mali katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini Nairobi.

Baadaye rais huyo atafanya mashauriano na rais Uhuru Kenyatta katika ikulu ya Nairobi.

Siku yan Jumapili rais Obama atahutubia mkutano wa wakuu wa mashirika ya kijamii katika chuo kikuu cha Kenyatta kabla ya kuhutubia mkutano mwingine kwa wakenya wote katika uwanja wa Kasakani.

Obama anatarajiwa kuondoka siku ya Jumapili kuelekea nchini Ethiopia.

Maelfu ya wakenya wamejipanga kando ya barabara kuu inayotoka uwanja wa ndege ili kumlaki rais huyo wa Marekani, ambaye anarejea nchini Kenya ambako babake alizaliwa.

Mamilioni ya Wakenya wengine naowalifuatilia kuwasili kwake kwenye runinga.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post