Utafiti_ WATOTO WAONGO NDIYO WENYE AKILI ZAIDI KULIKO WASIODANGANYA

 

Wanasayansi nchini Uingereza wanasema kuwa wana ushahidi kwamba watoto wanaodanganya bila mtu kugundua wana kumbukumbu nzuri ikilinganishwa na wale wasiodanganya.

Watafiti katika chuo kikuu cha Sheffield kwa siri walichukua filamu ya watoto wa umri wa miaka sita na saba wakifanya mtihani uliokuwa na majibu ambayo yalikuwa yameandikwa nyuma ya zao.

Wale waliodanganya kuhusu kile waliochofanya walifanya vyema kutokana na uwezo wao kukumbuka walichofunzwa.

Mmoja ya watafiti hao Elena Hoicka alisema kuwa sababu kuu ni kwamba wale wanaodanganya hulazimika kukumbuka ukweli wote pamoja na uongo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post