Taarifa Rasmi!! BANZA STONE HAJAFARIKI DUNIA,FAMILIA YASIKITISHWA NA UZUSHI WA WANAMITANDAO YA KIJAMII,SIKILIZA HAPA SAUTI

Familia ya Mwanamuziki  Banza Stone imekanusha taarifa zinazozidi kusambaa  kwenye mitandao ya kijamii kuhusu kifo cha msanii Banza Stone.


Akiongea na Malunde1  Blog hivi punde,Kaka wa msanii huyo Jabir Ally Masanja anayepatikana kwa simu namba 0753-786016  amesema kuwa mdogo wake ni mzima,tangu jana atoke hospitali yupo nyumbani kwao Sinza Vatican,hali yake ni nzuri anaendelea vyema na anazungumza.

Jabir amesema tangu jana usiku amepokea simu nyingi sana kuhusu taarifa hizo ikiwa ni pamoja na kupewa pole na watu kufika nyumbani.

Amesema taarifa hizo siyo za kweli kwani Banza Stone ni mzima kabisa.

"Tumepata hizi taarifa za kizushi jana saa tatu usiku,Tumepata usumbufu sana,hatujalala kabisa,ukweli ni kwamba kaka yangu ni mzima,anaongea,nasikitika sana kwanini watu wanazusha taarifa za uongo,sijui kwanini watu wanafanya vitu kama hivi,inasikitisha sana,watu wa mitandao ni vyema wakawa na uhakika wa vitu wanavyopost siyo kukurupuka tu",amesema Jabir.

MSIKILIZE HAPA JABIR AKIZUNGUMZA NA MALUNDE1 BLOG HIVI PUNDE.....

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post