Noma Sana!! GARI LIKIENDESHWA NA WATU WAWILI LAPARAMIA NYUMBA NA KUINGIA CHUMBANI SHINYANGA




Kumetokea ajali ya aina yake jioni hii mjini Shinyanga ambapo gari ndogo aina ya RAV4 yenye namba za usajili T167 ATW imegonga nyumba katika eneo la Mnara wa Voda karibu na ofisi za CHADEMA mjini Shinyanga.


Tukio hilo limetokea leo majira ya saa 11 jioni ambapo mashuhuda wa tukio hilo wameiambia Malunde1 blog kuwa gari hiyo ilikuwa inaendeshwa na watu wawili wanaodaiwa kuwa walikuwa wanajifunza kuendesha tena kwa mwendo kasi ndipo gari ikawashinda na kupoteza mwelekeo kisha kugonga nyumba hiyo na kusababisha uharibifu mkubwa.

Gari hiyo imeharibu vibaya Chumba cha mpangaji aliyejulikana kwa jina la Fatuma kuharibu vifaa mbalimbali zikiwemo TV katika chumba hicho na chumba cha jirani cha Fundi Sonara aliyejulikana kwa jina la Ally Salum.

Hata hivyo hakuna mtu aliyepoteza maisha wala kujeruhiwa na wahusika wanashikiliwa na jeshi la polisi kwa uchunguzi zaidi na mmliki wa gari hiyo bado hajajulikana.

Mwandishi wetu Kadama Malunde,alifika eneo la tukio,ametuletea picha zifuatazo

Gari ikiwa imegonga nyumba hiyo
Gari ikiwa chumbani
Muonekano wa gari hiyo kwa ukaribu
 

Askari wa usalama barabarani wakiwa eneo la tukio wakiwajibika
Gari ikiwa ndani ya chumba
 

Mashuhuda wa tukio hilo wakiwaeleza  askari polisi wa usalama barabarani namna ajali hiyo ilivyotokea
Katikati ya hiyo miti ndipo ilipopita gari hiyo ikiwa katika mwendo kasi kisha kugonga nyumba hiyo
 
 ndani ya chumba cha mpangaji Fatuma

Chumba cha mpangaji Fatuma kikiwa kimeharibika vibaya
Fundi Sonara Ally Salum akionesha ilipokuwa TV yake iliyoharibika

Fundi Sonara Ally Salum akionesha akitafakari jambo nje ya chumba chake

Askari wakitafakari namna ya kuiondoa gari hiyo eneo la tukio
Wakazi wa Shinyanga wakiwa eneo la tukio baada ya gari hiyo kuondolewa kwenye chumba
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post