MBUNGE WA SHINYANGA MJINI STEPHEN MASELE AMTOSA LOWASSA SAKATA LA URAIS TANZANIA

Mbunge wa Jimbo la Shinyanga mjini, Stephen Masele (kulia) akisalimiana na Naibu waziri wa fedha nchini, Mwigulu Nchemba muda mfupi mara baada ya (Nchemba) kuwasili katika ofisi za CCM Shinyanga mjini, wakati Nchemba alipokuwa akitafuta wanachama wa CCM wa kumdhamini. Kulia mwanzoni ni mmoja wa wajumbe wa kamati ya siasa, Rajabu Abasi -Picha na Suleiman Abeid



Mbunge wa Jimbo la Shinyanga mjini, Stephen Masele ametoa ufafanuzi kuhusiana na madaiya kumuunga mkono mmoja wa makada wa Chama cha Mapinduzi (CCM), wanaowaniakugombea urais kwa tiketi ya CCM na kukanusha habari zilizoandikwa nabaadhi ya vyombo vya habari vilivyodai amejiunga kwenye kambi ya MheshimiwaEdward Lowassa. 

Masele ambaye pia ni Naibu waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) alitoaufafanuzi huo juzi alipokuwa akimkaribisha kada mwingine wa CCM, MwiguluNchemba aliyefika katika ofisi za CCM Shinyanga mjini kwa ajili ya kutafutawana CCM wa kumdhamini ili aweze kuteuliwa kugombea urais kwa tiketi ya CCM. 

AkifafanuaMasele alisema yeye kama mbunge wa Jimbo la Shinyanga mjini ni wajibu wake pamojana viongozi wengine wa CCM wilayani humo kuhakikisha wanamsaidia kada ye yotewa chama anayekwenda kwa ajili ya kutafuta wadhamini na hakuna mtu anayemuunga mkono miongoni mwa waliotangaza nia ya kugombea urais kwa vile
wote ni wake. 


“Sisi kama wajumbe wa kamati ya siasa ni wajibu wetu kuandaa mazingira mazuri kwa watangaza nia wetu na makada wenzetu wote wanaokuja katika eneo letu hili, na mimi kama mbunge ninao wajibu kabisa wa kushiriki kikamilifu kuhakikisha kwamba mambo yote yanakuwa sawasawa, nawapongeza wale wote mliojitokeza kumdhamini pia mwenzetuMwigulu Nchemba,”.

 “Sisi huku wengine siyo wajumbe wa NEC na walasiyo wajumbe wa Kamati kuu, lakini ni wajumbe wa mkutano mkuu wa CCM Taifa, kazi yetuni kusubiri vikao vya juu vya chama vifanye kazi yake na hatimae vitatuletea mgombea wa CCM na tutapigana kufa na kupona kuhakikisha chama chetu kinashinda,”alieleza Masele. 

 Kwa upande wake kada wa CCM na Naibu waziri wa fedha, Mwigulu Nchemba akizungumza na wanachama wa CCM 45 waliojitokeza kumdhamini wakiwemo wazee maarufu wa mjini Shinyanga alisema moja ya lengo lake kuu la kutaka kugombea nafasi ya urais waJamhuri ya Muungano wa Tanzania ni kuwavusha watanzania kuelekea katika taifa lenye uchumi wa kati. 

Mwigulu alisema anaamini mgombea wa CCM ndiye atakayeibuka na ushindi mkubwa katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 25, mwaka huu na kwamba wanachosubiri watanzania walio wengi hivi sasa ni kuona chama chake kinampa ridhaa ya kupeperusha bendera yaCCM ili waweze kumchagua.

 “Vyanzo vyangu vya habari na taarifa mbalimbali zinaonesha watanzania wengi wanasubiri chama changu kinipe ridhaa ya kupeperusha bendera ili wao waweze kuunga mkono agenda yao  waliyoiona tangu nilipotangaza nia ya kugombea urais, sina mashaka ndani ya chama na nje ya chama kwamba agenda ya watanzania ikishindanishwa na jambo lolote itashinda tu,”

 “Kwa wana CCM, CCM inapata uhalali wa kuongoza taifa letu kwa aina tatu ikiwemokutoka urithi wa vyama vilivyokomboa taifa letu, pili kwa kazi ilizozifanya kwakuunda serikali tangu ilipoanzishwa mpaka hivi sasa na kazi zakuliletea taifa hili maendeleo tangu ilipoanzishwa mpaka hivi leo, na pia sifa yatatu ni kwa kazi inazotarajia kwenda kuzifanya sasa,” alieleza Nchemba.

 Aidha kada huyo wa CCM alirejea kauli zake za awali kwa kueleza kuwa moja ya agenda yakekuu atakapofanikiwa kuingia Ikulu ni kuifanya Tanzania kuwa nchi ya kipato chakati pamoja na watanzania wenyewe kuwa watu wa nchi ya kipato cha kati na waondokane na kauli ambayo wameisikia muda mrefu ya uchumi kukua huku wao wakiona umasikini ndiyo unaokua. 

Katika hatua nyingine Mwigulu alikanusha madai kwamba kitendo cha kujitokeza idadikubwa ya makada wa CCM kutaka kuteuliwa kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itakuwa ni chanzo ya chama hicho kusambaratika baada ya majina yamakada wengi kukatwa wasiweze kugombea nafasi hiyo.

 “Si kweli kwamba eti CCM itasambaratika mara baada ya uteuzi wa mgombea wake katikanafasi ya urais wa Jamhuri ya Muungano, tupo imara na tutaendelea kuongoza nchihii, hatuwezi kusambaratika, maana watanzania hawataangalia sura ya mtu,wataangalia agenda kuu watakayoisimamia ili kuifanya nchi kuwa ya uchumi wakati,” alieleza Nchemba. 

Aidha alitoa wito kwa wana CCM katika dua zao zote kuhakikisha wanatafuta mgombea waCCM anayetokana na CCM na siyo yule mgombea aliyepitia CCM na kwamba yeye mwenyewe anaamini amejitokeza katika wakati sahihi na kwa mahitaji sahihi yawatanzania na kwamba anaamini akichaguliwa kuwa rais atawavusha. 

Na Suleimna Abeid-Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post