ANGALIA PICHA_WATU WATATU WANAODAIWA KUWA AL SHABAAB WAMEUAWA KATIKA MAPAMBANO NA POLISI HUKO MOROGORO

Morogoro Maulid Kambaya June 27 2015

Watu watatu wamefariki wawili kati yao wanasadikiwa kuwa ni wafuasi wa Al Shabaab katika mapigano baina yao na jeshi la Polisi mkoa wa Morogoro.

Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro amesema tukio hilo limetokea eneo la mpakani mwa mkoa wa Morogoro wilaya ya Mvomero na mkoa wa Tanga ambapo watu hao walikuwa wamejificha msituni.

Amesema jeshi hilo linawashikilia watu sita kwa kuhusika na tukio hilo, na kwamba uchunguzi zaidi unafanyika ikiwa ni pamoja na msako mkali katika eneo hilo.

Taarifa kutoka katika hospitali ya mission ya Turian mkoani Morogoro zinasema kuwa maiti tatu zimehifadhiwa hapo ambapo kati ya hizo, maiti mbili zinaonekana kuwa ni za watu wasio raia wa Tanzania huku moja ikiwa ni ya mtu ambaye alijeruhiwa vibaya na badaye kufariki akiwa hospitalini hapo.
Via>>EATV

Mtangazaji na Mwandishi wa habari wa Radio One Maulid Kambaya kwenye page yake ya Facebook alipost picha za walivyokamatwa navyo ‘Magaidi’ hawa.
Morogoro Maulid Kambaya June 27 2015
Morogoro 4
Morogoro 3
Morogoro 2

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post