ANGALIA PICHA_ WANANCHI WAGOMBANIA KUMZIKA MUFTI SIMBA MJINI SHINYANGAKatika hali ambayo iliyotafsiriwa kuwa shehe mkuu wa Tanzania Mufti Issa Shaaban bin Simba alikuwa kipenzi cha watu,jana wakati wa mazishi yake,maelfu ya wakazi ndani na nje ya mkoa wa Shinyanga walijitokeza kumsindikiza mpendwa wao katika nyumba yake ya milele katika makaburi ya Waislam ya Nguzo nane mjini Shinyanga.
 
Katika hali isiyokuwa ya kawaida waombolezaji walijipanga kuanzia nyumbani kwa marehemu mtaa wa Majengo hadi kwenye makaburi ya Nguzo Nane mjini wakisubiri kubeba mwili wa marehemu mufti Simba.
 
Mbali na maelfu ya watu kufurika nyumbani kwa marehemu mtaa wa Majengo,pembezoni mwa barabara,wakazi wa Shinyanga waligombania kuingia katika makaburi ya Nguzo nane pamoja na kwamba askari wengi wa jeshi la polisi walitanda eneo hilo kuimarisha ulinzi.

Wakazi wa Shinyanga walilazimika kusukumana na polisi huku wengine wakilazimika kupanda juu ya miti ili kuona kilichokuwa kinaendelea wakati wa mazishi hayo.Picha zote na Kadama Malunde- Malunde1 blog
 ANGALIA PICHA HAPA CHINI UONE HALI ILIVYOKUWA

Wananchi wakisaidia na polisi kuzuia wananchi wasiingie katika makaburi ya Nguzo nane kwani nafasi ilikuwa haitoshi
Wakazi wa Shinyanga wakiwa wamening'inia kwenye ukuta unaozunguka makaburi ya Nguzo nane
Wakazi wa Shinyanga wakiwa katika makaburi ya Nguzo nane,wengine waliambuliwa kupanda kwenye miti na ukuta uliopo katika makaburi hayo

Kaburi la Mufti Simba

Msafara wa rais Jakaya Kikwete aliyeongoza mazishi ya mufti Simba ukiondoka makaburini,huku wakazi wa Shinyanga wakiwa pembezoni mwa barabara karibu na soko la Nguzo nane

Picha zote na Kadama Malunde- Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post