Inatisha SANA_ AVAMIWA NA FISI WA KICHAWI HARUSINI,ANYOFOLEWA PUA NA MDOMO,ANAHITAJI MSAADA WAKO


Sophia  Mashala( 29) mkazi wa kijiji cha Kishapu wilayani Kishapu aliyenyofolewa pua na mdomo na fisi anayedaiwa kuwa ni wa kishirikina

Sophia  Mashala( 29) akiongea kwa tabu kutokana na mdomo na pua yake kuliwa na fisi
Makovu mbalimbali aliyoyapata Sophia baada ya kuvamiwa na fisi harusini


Hujafa Hujaumbika! Unaweza ukawa mzima leo kesho tukasikia mengine.Sophia  Mashala( 29) mkazi wa kijiji cha Kishapu wilayani Kishapu amekuwa katika mateso kwa miaka mitano sasa baada ya kujeruhiwa vibaya na Fisi akiwa kwenye sherehe ya mtoto wa Shemeji yake iliyokuwa inafanyika katika kitongoji cha Nyalusanga kijiji cha Kishapu kisha kunyofolewa pua.

Sophia anasema siku ya tukio akiwa kwenye harusi na wenzake zaidi ya 30 tarehe 16,  Oktoba 2011,siku ya Jumamosi  majira ya saa 12 jioni,ghafla alijitokeza fisi na kumvamia yeye tu kisha kumshambulia sehemu mbalimbali za mwili wake huku mdomo na pua yake vikinyofolewa.

Anahitaji msaada wa shilingi milioni 2 na laki tano ili afanyiwe upasuaji kwani sasa Anapumulia mdomoni,anakauka koo,mafua yanatokea mdomoni na kusumbuliwa na vichomi.

Tangu kutokea kwa tukio hilo la fisi anayedaiwa kuwa wa kichawi ametelekezwa na mume wake wa ndoa Solomoni Dilu aliyezaa naye watoto wawili ambaye sasa ameamua kuoa mke mwingine huku vitu vyote  aliyevyochuma naye akinyang’anywa na kutojali hata watoto wake.

Sophia anasema awali aliolewa kwa mahari ya ng’ombe zaidi ya 15 baada ya kupata matatizo hayo  wakwe zake walimtenga huku wakikataa kutoa pesa za  matibabu kwa madai atamaliza mahari aliyotolewa hivyo atafute sehemu nyingine atakapopata pesa za matibabu.

Sophia amezunguka katika hospitali mbalimbali nchini kutafuta matibabu wakati huo huo kutafuta haki katika vyombo vya sheria lakini anadai hakuna mafanikio yoyote aliyopata kutokana na kesi yake kupigwa kalenda kila kukicha mahakamani.


Kutoa ni moyo,wasiliana na Sophia  kwa simu namba 0768 718 846 au 0719 213 460


MSIKILIZE HAPA AKISIMULIA JINSI ALIVYOPATA TUKIO NA KINACHOMSUMBUA HIVI SASA

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post