IDADI YA WATU WALIOFARIKI KUTOKANA NA JOTO YAFIKIA 700 HUKO PAKISTAN

null 


Waziri mkuu nchini Pakistan Nawaz Sharrif ametaka hatua za dharura kuchukuliwa huku idadi ya watu waliofariki kutokana na wimbi la joto katika mkoa wa kusini wa Sindh ikifikia 700.

Mamlaka ya kukabiliana na majanga ya dharura NDMA imesema kuwa imepokea maagizo kutoka kwa Nawaz Sharrif kuchukua hatua za dharura.

Jeshi tayari limepelekwa katika eneo hilo kujenga vituo vya kukabiliana na joto hilo ili kuisaidia mamlaka hiyo.

Wengi wa waathiriwa ni watu wazima kutoka kwa familia zinazopata mapato ya chini.

Maafisa wa afya wanasema vifo vingi vimetokea katika mji mkuu wa Karachi ambao ulikumbwa na joto la viwango vya juu vya hadi digree 45 c.

Katibu wa afya katika mkoa wa Sindh Saeed Mangnejo amesema kuwa watu 612 walifariki katika hospitali kuu ya serikali mji huo katika kipindi cha siku nne zilizopita.

 Wengine 80 wameripotiwa kufariki katika hospitali za kibinafsi.
Via>>BBC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post