Duh!! Hii Kali!! JAMAA AUA MKE WAKE ETI KISA ANAONGEA SANA!!

Mara nyingi imezoeleka ndani ya nyumba wanawake wengi huwa na tabia ya kuongea sana kuliko wanaume kitendo ambacho mara nyingine kinawachukiza baadhi ya wanaume na kuamua kuchelewa kurudi nyumbani ili kuepukana na kelele za wake zao.

Jamaa mmoja katika jimbo la Texas, Marekani anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kusababisha mauaji baada ya kumziba mke wake Ceaira Ford na mto hadi kufa kwa madai anaongea sana.

Baada ya kufanya kitendo hicho Janathamn Edelen alijipeka mwenyewe kituo cha polisi na polisi walipokwenda nyumbani kwake walishuhudia mwili wa mwanamke huyo ukiwa juu ya kitanda huku tayari akiwa amefariki.

Mwanaume huyo amehukumiwa kwenda jela na kulipa faini ya dola 500,000.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post