Taarifa Kamili_KIFO CHA MUFTI MKUU WA TANZANIA SHEIKH ISSA SIMBA NA RATIBA YA MAZISHI


Mufti  Shekh  Mkuu wa Tanzania, Issa Bin Shaaban Simba enzi za uhai wake
Sheikh Mkuu wa Tanzania, Mufti Shaban Bin Simba amefariki dunia leo katika hospitali ya TMJ Jijini Dar es Salaam.

Akithibisha kutokea kwa kifo hicho, Kaimu Kiongozi wa shughuli za serikali bungeni Mh Mary Nagu amesema msiba huo umetokea leo asubuhi na kwamba marehemu alikuwa akisumbulia na kisukari na shinikizo la moyo kwa muda mrefu.

Mh. Nagu amesema serikali inaungana na waislamu wote kuomboleza msiba huo, na kumuelezea marehemu kwamba alikuwa ni kiungo muhimu kati ya waislamu na serikali.

Baraza la Waisilamu Tanzania BAKWATA limesema kesho mwili wa marehemu utaagwa jijini Dar es salam  na mazishi yatafanyika siku ya Alhamis mkoani Shinyanga.

‪#‎RIPShabanSimba‬ Inna Lillahi Wainna Ilaihi Rajiun
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post