BIBI HATAKI MPANGAJI AJIFUNGULIE KWENYE NYUMBA YAKE,BINTI KALETA UBISHI KILICHOFUATA NI STORI.......

SAD WOMAN

Heka heka imetokea Shinyanga ambapo Bibi mmoja kaachiwa nyumba na marehemu mume wake, lakini masharti yake hataki mpangaji wake ajifungulie nyumbani kwake na wala hataki mtoto mchanga nyumbani kwake.

Akisimulia mkasa huo mmoja wa wapangaji wake ambaye alifikiwa na mtoto huku bibi huyo bila huruma akimzuia kuingia ndani ya nyumba yake kwa ajili ya taratibu za mazishi alisema amesikitishwa sana na kitendo hicho kwa kuwa si cha kibinadamu.

Alisema aliopanga kwa bibi huyo tangu mwaka 2013 na alipewa masharti ya kutokuwa na watoto na hata alipobeba mimba alikwenda kujifunguliwa kwao na kukaa kwanza hadi mtoto alipokuwa mkubwa kidogo kisha kurejea ingawa bibi huyo hakutaka arudi na mtoto wake.

Mtoto huyo aliugua gafla na kufariki dunia lakini cha kushangaza bibi huyo alimfukuza na kukataa maiti kuingizwa nyumbani kwake hivyo kuwalazimu kupeleka msiba kwa Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa.

Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa Rashid Abdalah alisema wapangaji wengi wamekua wakimlalamikia bibi huyo kwa kuwafukuza wanapokuwa wajawazito na alidai marehemu mume wake aliweka zindiko ndani ya nyumba hiyo.

Kitendo cha bibi huyo kiliwakasirisha watu ambao walijazana nyumbani kwake kutaka kujua sababu ya yeye kufanya hivyo, lakini bibi huyo alionekana kuwa na jazba huku akiwafukuza na kutotaka kuwasikiliza.

Hekaheka iko hapa, utasikia wahusika wote wakisimulia mkasa ulivyokuwa.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post