ANGALIA PICHA- BENKI YA CRDB YATOA MSAADA WA MADAWATI 100 SHULE YA MSINGI MWENGE


Hapa ni katika Shule ya Msingi Mwenge mjini Shinyanga ambako Mkuu wa wilaya ya Shinyanga bi Josephine Matiro amekabidhi madawati 100 yaliyotolewa na Benki ya CRDB tawi la Shinyanga kufuatia jitihada za mstahiki meya wa manispaa ya Shinyanga Gulam Hafeez Mukadam kuomba msaada kwa benki hiyo ili kuwanusuru wanafunzi 1180 wa shule hiyo kongwe iliyojengwa mwaka 1935 kusoma wakiwa wamekaa chini( sakafuni) pamoja na kwamba shule iko mjini

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza muda mfupi baada ya kuwasili katika shule ya msingi Mwenge kwa ajili ya kukabidhi madawati 100 yaliyotolewa na benki ya CRBD tawi la Shinyanga katika shule ya msingi Mwenge iliyopo katika manispaa ya Shinyanga-Aliyesimama kulia ni mwenyekiti wa kamati ya Shule ya msingi Mwenge bwana Abdalah Shekha

Wanafunzi wa Shule ya Msingi Mwenge wakiwa shuleni wakati wa zoezi la kukabidhiwa madawati 100
Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Mwenge Mahamudu Ibrahimu akisoma risala-Alisema hivi sasa shule hiyo ina jumla ya wanafunzi 1180,wavulana 561 na wasichana 619,walimu 25 wa kiume wanne na wa kike 21.

Walimu na viongozi wa kata ya Shinyanga mjini wakiwa eneo la tukio-Mwalimu huyo mkuu wa shule ya msingi Mwenge alisema shule hiyo kongwe zamani ikijulikana kwa jina la "Indian School" hivi sasa inakabiliwa na changamoto mbalimbali kama vile upungufu wa vyumba vya madarasa,walimu,madawati 214 na matundu ya vyoo.
Meya wa manispaa ya Shinyanga ndugu Gulam Hafeez Mukadam ambaye ni diwani wa kata ya Shinyanga Mjini,akizungumza katika shule ya msingi Mwenge ambapo alisema aliwahi kusoma katika shule hiyo.Alisema kutokana na changamoto ya watoto kukaa chini wakati wa masomo hivi karibuni aliamua kuanza kutafuta wafadhili ili kuwanusuru wanafunzi hao,akaonana na uongozi wa benki ya CRDB ambao walikubali kutoa msaada madawati 100

Meya wa manispaa ya Shinyanga ndugu Gulam Hafeez Mukadam aliushukuru uongozi wa benki ya CRBD kwa kuona umuhimu wa kusaidia katika sekta ya elimu nchini huku akiwaomba kuendelea na moyo wa kusaidia shule za manispaa hiyo na mkoa kwa ujumla kwani zinakabiliwa na changamoto nyingi

Baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Mwenge wakiwa eneo la tukio wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea

Mwenyekiti wa kamati ya Shule ya msingi Mwenge bwana Abdalah Shekha akizungumza wakati zoezi la kukabidhi madawati hayo 100 yaliyotolewa na Benki ya CRDB,ambapo hakusita kuonesha furaha yake kwa benki hiyo kuwapunguzia mzigo wa upungufu wa madawati,ambapo baada ya msaada huo sasa wanapungukiwa madawati 214 hivyo kuhitaji msaada zaidi

Meneja wa Benki ya CRDB mkoa wa Shinyanga ndugu Said Pamui akizungumza wakati wa kukabidhi madawati 100.Alisema benki hiyo iliguswa na kusikitishwa na kitendo cha wanafunzi waliopo katikati ya mji kukaa sakafuni wakati wa masomo hivyo kuamua kutoa msaada huo kwa ajili ya kuendeleza sekta ya elimu nchini

Meneja wa Benki ya CRDB mkoa wa Shinyanga ndugu Said Pamui alisema pamoja na kuwekeza kwenye elimu,aliwataka wazazi kuejnga utamaduni wa kuwawekea akiba watoto kupitia akaunti ya watoto "Junior Account" inayopatikana katika benki hiyo ambayo haina gharama kubwa za kufungua na kuiendesha ili kuwasaidia watoto wao kwa mahitaji ya shule,afya,sare n.k

Wazazi na walezi wa wanafunzi wa shule ya msingi Mwenge wakiwa enep la tukio wakimsikiliza meneja wa benki ya CRBD mkoa wa Shinyanga.

Meneja wa Benki ya CRDB Said Pamui alisema benki yake sasa inatoa fursa  ya Bima ya afya kwa wafanyakazi wasio watumishi wa serikali inayotolewa kwa shilingi 80,640/= tu na unapata fursa ya kutibiwa mahali popote nchini mwaka mzima

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga ndugu Josephine Matiro akikata utepe wakati wa kukabidhi madawati 100 yaliyotolewa na benki ya CRDB mkoa wa Shinyanga leo katika shule ya msingi Mwenge iliyopo mjini Shinyanga

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga akizungumza wakati wa zoezi la kukabidhi madawati hayo ambapo aliipongeza benki ya CRDB kutoa msaada huo huku akizitaka benki zingine na taasisi mbalimbali zilizopo katika wilaya ya Shinyanga kujitokeza na kutoa msaada kwa jamii,hususani katika shule kwani nyingi zinakabiliwa na changamoto kadha wa kadha
Miongoni mwa madawati yaliyotolewa na benki ya CRDB.Katika mikakati ya kupunguza muda wa kupata huduma za kibenki kwa wateja wake,sasa wananchi wanaweza kupata huduma hizo kupitia mawakala wao waliotapakaa kila kona lakini pia kupitia huduma ya Sim Banking wateja wanafurahia huduma za benki hiyo 
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro ambaye pia ni Mwalimu, alisisitiza pia umuhimu wa wananchi kushiriki katika shughuli mbalimbali za maendeleo kutokana na kwamba serikali pekee haiwezi kumaliza changamoto zilizopo mashuleni.Alisema msingi mkuu wa watoto ni elimu hivyo kuwataka wanafunzi kuwasikiliza walimu wao na kuzingatia wanayofundishwa darasani
Walimu wa shule ya msingi Mwenge wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea....
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro alisema katika ziara yake wilayani humo tangu alipohamishiwa wilaya ya Shinyanga mwezi Machi mwaka huu,amebaini kuwa wanafunzi wengi wanakaa chini hivyo kupitia mikutano yake ameagiza kuwepo kwa ushirikiano kati ya wazazi na shule ili kuhakikisha changamoto hizo zinaondolewa
Afisa elimu Vifaa na Takwimu msingi bwana Paul Magubiki kwa niaba ya mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga akizungumza katika shule ya msingi Mwenge,ambapo alipongeza jitihada za meya wa manispaa ya Shinyanga kutafuta wafadhili kwa ajili ya kuwasaidia wanafunzi wa shule hiyo

Baada ya zoezi la kukabidhi madawati hayo,Mstahiki meya wa manispaa ya Shinyanga Gulam Hafeez Mukadam akicheza muziki na wanafunzi wa shule ya msingi Mwenge

Shule ya msingi Mwenge ilijengwa mwaka 1935,ikafunguliwa mwaka 1938 wakati huo ikijulikana kwa jina la "Indian School" na mwaka 1970 ikakabidhiwa kwa serikali na imekuwa na maendeleo mazuri kielimu pamoja kugubikwa na changamoto nyingi kama vile upungufu wa madawati,madarasa,walimu na matundu ya vyoo.

Picha zote na Kadama Malunde- Malunde1 blog 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post