ANGALIA PICHA- MAKONGORO NYERERE AREJESHA FOMU YA KUGOMBEA URAIS MKOANI DODOMA

Mheshimiwa Makongoro Nyerere akikabidhi
fomu ya kugombea urais kupitia Chama Cha Mapinduzi(CCM) kwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Rajab Luhavi (kushoto) katika ofisi za makao makuu ya CCM mkoani Dodoma leo baada ya kumaliza zoezi la kukusanya saini za wadhamini katika mikoa mbalimbali nchini
                                                 **************
Mtoto wa Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere, Makongoro Nyerere, leo amerejesha fomu ya kugombea urais kupitia Chama Cha Mapinduzi(CCM) baada ya kumaliza zoezi la kukusanya saini za wadhamini.
Makongoro ambaye jana alihitimisha zoezi la kukusanya saini za wadhamini mkoani Shinyanga, amekusanya saini za wadhamini katika mikoa yote 30 ya Tanzania.
Akizungumza na Malunde1 blog , Makongoro amesema amemaliza hatua ya kwanza ya safari yake ya kuwania kwenda Ikulu hivyo hatua ya pili anamuachia Mwenyezi Mungu kuiangazia safari yake ya kwenda Ikulu.
“Nimemaliza zoezi la kukusanya saini za wadhamini nchi nzima…leo nimereshesha fomu zangu kwa ajili ya kusubiri utaratibu mwingine wa kichama, hatua hii mwenyezi Mungu ndiye anajua muelekeo wangu wa mbio hizi"-Makongoro
 ANGALIA PICHA HAPA CHINI WAKATI MAKONGORO AKIKABIDHI FOMU LEO









Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post