ANGALIA PICHA_ JINSI MTANGAZA NIA YA URAIS MKULIMA WA DARASA LA 7 ALIVYOWASILI SHINYANGA KUCHUKUA WADHAMINI WAKEHapa ni katika ofisi za Chama Chama Mapinduzi (CCM) wilaya ya Shinyanga mjini.Pichani katikati ni mtangaza nia kuwania urais nchini Tanzania katika uchaguzi mkuu ujao kupitia CCM,Lidephonce Bilohe,ambaye ni mkulima mwenye elimu aya darasa la saba akisaini fomu ya majina ya wadhamini 30 aliopata katika mkoa wa Shinyanga.Picha zote na Kadama Malunde- Malunde1 blog


Bilohe ambaye ni mkulima amesema amekaa muda mrefu katika chama akitamani kuwa rais wa nchi na matarajio yake ni ushindi kutokana na uwezo na uzoefu wake ndani ya chama pamoja na kwamba elimu yake ni darasa la saba.

Kushoto ni mbunge wa Jimbo la Shinyanga mheshimiwa Stephen Masele ambaye ni Naibu waziri ofisi ya makamu wa rais Mazingira,akizungumza katika ofisi za CCM wilaya ya Shinyanga mjini ambapo pamoja na mambo mengine alimtakia kila kheri mtangaza nia huyo ndugu Bilohe katika harakati zake za kusaka urais

Mheshimiwa Stephen Masele akishikana mkono na mtangaza nia kuwania urais nchini Tanzania kupitia CCM Lidephonce Bilohe

Lidephonce Bilohe amepata wadhamini 30 kutoka mkoa wa Shinyanga na kuwaahidi watanzania kumuunga mkono kwani anayo nia dhabiti ya kuwaongoza wananchi.

Mtangaza nia Lidephonce Bilohe akiwapungia,ambaye anafanya ziara ya kusaka wadhamini peke yake, mkono wakazi wa Shinyanga nje ya ofisi za CCM wilaya ya Shinyanga mjini leo.Picha zote na Kadama Malunde- Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post