WANAFUNZI WA UDSM WAGOMA KUINGIA DARASANI KWA MADAI YA KUTOPEWA FEDHA ZA KUJIKIMU

Maelfu ya wanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es Salaam sehemu ya Mlimani wameanza mgomo kuingia darasani kwa madai ya kutopewa fedha za kujikimu kwa zaidi ya wiki 11 huku wakitaja gharama za maisha zikiwa zimepanda mara dufu.


Wakiongea katika viwanja vya chuo kikuu jijini Dar es Salaam kwa kile walichokiainisha kuwa ni njaa kali pamoja na kueleza kuendelea na mgomo hadi fedha zitakpoingia kwenye akaunti zao wametaja serikali kuchelewesha fedha hizo kupitia bodi ya mikopo kuwa ni kuwadhoofisha kimasomo.

 
Kwa upande wake makamu mkuu wa chuo kikuu cha Dar es Salaam Prof. Rwekaza Mukandara pamoja na kukiri madai ya wanafunzi elfu saba kati ya zaidi ya elfu kumi wanaofadhiliwa na serikali kupitia bodi ya mikopo kucheleweshewa fedha zao kuwa ya msingi amesema tayari amezungumza na bodi ya mikopo ambao wamemwahidi kuleta fedha zao haraka iwezekanavyo na kuwaomba wanafunzi kurejea madarasani kuendelea na masomo.


 
Wakati huo huo takribani wanafunzi 400 wa chuo kikuu cha Mt. Joseph cha Mbezi jijini Dar es Salaam mwaka wa kwanza wamesimamishwa masomo kwa muda usiojulikana baada ya kugoma kuingia madarasani wakidai fedha za kujikim kutoka bodi ya mikopo tangu mwezi Desemba mwaka jana hadi sasa wakieleza kuishindwa kuendesha maisha yao ya shule na kuhimili mazingira ya kupangha nyumba mitaani.


 
Katika taarifa ya kusimamisha wanafunzi hao iliyotolewa na makamu mkuu wa chuo cha Mt.Josephu Bw.Loyola Proteep aliyeambatana na mkuu wa wanafunzi maarufu kama Dean anakiri madai ya wanafunzi hao kuwa ya msingi na kuongeza kuwa waliwaomba utulivu na kuingia Madarasani wakati wakifuatilia madai yao bodi ya mikopo bila ya mafanikio na uongozi kuchukua uamuzi wa kuwasimamisha wanafunzi wote wa mwaka wa kwanza hadi vikao vya bodi vitakapoamua vinginevyo.

Via>>ITV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post