ALICHOKISEMA RAIS NYUSSI WA MSUMBIJI KUHUSU VITA YA UGAIDI NA UFISADI AKIWA BUNGENI TANZANIA

Rais wa jamhuri ya Msumbiji Filipe Nyussi amesema vita dhidi ya ugaidi na ufisadi ni vita ambayo inatakiwa kupigana kwa pamoja hivyo uhusiano mzuri uliopo kati ya Tanzania na nchi yake ukitumika vyema utaweza kumudu vita hiyo.


Mh Nyussi ametoa rai hiyo bungeni mjini Dodoma alipokuwa anahutubia wabunge ambapo amesema ili kupambana na umaskini katika nchi hizi mbili jambo kubwa ni kufanya kazi kwa pamoja na kila mmoja kumuheshimu mwenzake, ambapo kabla ya hotuba hiyo ametembelea makao makuu ya chama cha mapinduzi.


 
Kwa upande wake spika wa bunge Mh Anne Makinda amemweleza rais Nyussi kuwa bunge lake liko bega kwa bega na serikali yake na kwamba wataendeleza ushirikiano uliopo kwa manufaa ya nchi zote mbili.
 


Mara baada ya hotuba yake bunge limeendelea utaratibu wake ambapo waziri wa nchi muungano Mh Samia Suluhu Hassan amewasilisha bungeni makadirio ya mapato na matumizi ya ofisi ya makamu wa rais kwa mwaka huu wa fedha na kueleza mafanikio yaliyopatikana katika awamu ya nne pamoja na namna ambavyo changamoto zilizopo zinavyoshughulikiwa.


 
Akisoma maoni ya kambi rasmi ya upinzani upande wa ofisi ya makamu wa rais muungano Mh Tundu Lissu yamedai kuwa maagizo ya kambi hiyo yaliyotolewa mwaka jana yamepuuzwa ambayo ni pamoja na utoaji wa taarifa kuhusu fedha zote zinazopelekwa Zanzibar kupitia hazina au mamlaka yoyote ziwasilishwe ofisi ya makamu wa rais muungano huku kamati nazo zikiwasilisha taarifa zake na kuitaka serikali kubomoa nyumba zote zilizojengwa kinyume na sheria katika fukwe za bahari na kingo za mito.

Via>>ITV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post