TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI TANZANIA YATOA RATIBA YA UCHAGUZI MKUU 2015!!


Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetoa ratiba rasmi kwa vyama vya Siasa na wananchi wote itakayotumika katika Uchaguzi Mkuu wa Serikali  unaotarajia kufanyika Oktoba mwaka huu.
 
Kwa mujibu wa taarifa iliyosainiwa na Mwenyekiti wa Tume hiyo  Jaji wa Rufaa (Mst.) Damian Lubuva imesema kuwa kwa Mamlaka waliyopewa kwa mujibu wa vifungu vya 35B(1), (3) (a), 37 (1) (a) na 46 (1) vya Sheria ya Taifa ya Uchaguzi,  Sura ya 343, shughuli za uchaguzi zinatarajia kuanza hivi karibuni.
 
Taarifa hiyo imefafanua kuwa  Uteuzi wa wagombea Urais, Ubunge na Udiwani unatarajia kufanyika Agosti 21, 2015, na  kampeni za Uchaguzi kwa wagombea hao zitatarajia kuanza Agosti 22 mpaka - Oktoba 24 mwaka huu.

Halikadhalika siku ya kupiga kura kwa wananchi wote inatarajiwa kuwa Oktoba 25, 2015 kwa wale waliojitokeza kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527