SUNGUSUNGU WA MANISPAA YA SHINYANGA WAPEWA PIKIPIKI KUKABILIANA NA MAUAJI YA ALBINO NA VIKONGWE

Katika kukabiliana na vitendo vya mauaji ya vikongwe na watu wenye ulemavu wa ngozi(albino),leo jeshi la jadi sungusungu katika halmashauri ya manispaa ya Shinyanga limekabidhiwa pikipiki yenye thamani ya shilingi milioni moja,laki 6 na elfu 50 kwa ajili ya kuimarisha ulinzi na usalama kwenye maeneo yao.Zoezi la makabidhiano limefanyika katika ofisi ya mkuu wa wilaya ya Shinyanga mgeni rasmi akiwa ni mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama katika wilaya hiyo-Picha zote na Kadama Malunde-Shinyanga

Pikipiki hiyo imetolewa na mstahiki meya wa manispaa ya Shinyanga Gulam Hafeez Mukadam kupitia kwa mfanyabiashara Ndegesela na kukabidhiwa kwa katibu wa jeshi la sungusungu manispaa ya Shinyanga James Deshi.Pichani katikati ni meya wa manispaa ya Shinyanga Gulam Hafeez Mukadam akikabidhi ufunguo wa pikipiki kwa mkuu wa wilaya ya Shinyanga bi Josephine Matiro ambaye naye alikabidhi ufunguo huo kwa katibu wa jeshi la sungusungu manispaa ya Shinyanga James Deshi.

Akikabidhi pikipiki hiyo meya wa manispaa hiyo Gulam Hafeez Mukadam alisema pikipiki hiyo itatumika katika kuimarisha ulinzi na usalama ikiwa ni pamoja na kukabiliana na mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi na vikongwe.

Zoezi la makabidhiano linaendelea

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro  akizungumza wakati wa zoezi la makabidhiano ambapo alisema ingawa katika manispaa hiyo hapajaripotiwa tukio la mauaji ya albino,pikipiki hiyo itatumika katika kuimarisha zaidi ulinzi kwa watu wenye ulemavu wa ngozi na vikongwe.

Matiro alisema wataendelea kutoa msaada wa pikipiki  kwa jeshi la sungusungu katika kata 17 za manispaa hiyo na mwezi Juni mbunge wa Shinyanga Mjini Stephen Masele atatoa pikipiki 2 kwa jeshi hilo

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akishikana mkono na  mwenyekiti wa sungu sungu  manispaa ya Shinyanga Shiganza Shidula

Nyuma ya pikipiki iliyokabidhiwa kwa jeshi la sungusungu
Katibu wa jeshi la sungusungu manispaa ya Shinyanga James Deshi akikagua pikipiki hiyo baada ya kukabidhiwa 
Viongozi wa Jeshi la Sungusungu halmashauri ya manispaa ya Shinyanga wakiondoka na pikipiki waliyokabidhiwa,anayeendesha ni katibu wa jeshi la sungusungu manispaa ya Shinyanga James Deshi-Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog Shinyanga



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post