KUHUSU TAARIFA YA MGAHAWA KUUZA NYAMA ZA BINADAMU HUKO NIGERIA

 

Idhaa ya kiswahili ya BBC imethibitisha kuwa taarifa tuliyochapisha kwamba kuna mgahawa mmoja nchini Nigeria unaouza nyama ya binadamu sio za kweli.

Tunaomba radhi kwa taharuki au hisia zozote zilizosababishwa na taarifa hiyo.

Tunaomba radhi kutokana na taarifa ambayo tuliichapisha hapa kuhusu mkahawa mmoja nchini Nigeria.Taarifa hiyo haikuwa sahihi na ilichapishwa bila kuzingatia utaratibu wa BBC. Tumeiondoa taarifa hiyo kwenye mtandao na tayari tumeanza uchunguzi kuthibitisha ni nini kilichosababisha taarifa kama hiyo kuchapishwa.


Tunazingatia kwa thamani kubwa sifa ya Idhaa ya Kiswahili ya BBC kama Idhaa inayozingatia uhakika wa habari zake na msimamo wa kutoegemea upande wowote na ni kwa sababu hiyo tunachukua hatua stahiki kuhakikisha kosa kama hilo halifanyiki tena.
Chanzo-BBC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post