Kali ya Mwaka!! MTOTO AWEKWA KWENYE BEGI NA KUSAFIRISHWA KAMA MZIGO

 

Mtoto mmoja wa miaka minane amesafirishwa hadi nchini Uhispania kutoka Morroco akiwa ndani ya sanduku kwa mujibu wa maafisa wa polisi wa Uhispania.
Mvulana huyo kwa jina Abou alipatikana ndani ya sanduku hilo lililokuwa limebebwa na msichana wa miaka 19 kuelekea Cueta,eneo lililo karibu na taifa la Morocco siku ya Alhamisi.

Wakati polisi walipolifungua sanduku hilo, mvulana huyo alikuwa katika hali mbaya sana.

Mvulana huyo kutoka Ivory Coast sasa anahudumiwa na mamlaka ya Cueta.

Gazeti la Uhispania El Paris liliripoti kwamba msichana huyo wa miaka 19 hana uhusiano na mtoto huyo na kwamba alilipwa na babaake ili kubeba sanduku hilo.

Babaake mtoto huyo anaishi katika visiwa vya Conary na kwamba alitarajia kuonana na mwanawe kulingana na gazeti hilo.

Chombo cha habari cha Uhispania Efe kimesema kuwa babaake mvulana huyo ambaye anajulikana kama Abou alisafiri hadi nchini Ivory Coast kumchukua mwanawe baada ya kuhamia katika eneo la Gran Canaria mwaka 2013.

Babaake baadaye aliripotiwa kumlipa raia huyo wa Morocco ambaye alimsafirisha mtoto huyo kupitia sanduku.

Msemaji wa polisi aliiambia Efe:''Alionekana kusita na kama ambaye hakutaka kupitia mpakani''.
Via>>BBC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post