Picha_EASYFLEX PRODUCTION YAJENGA CHOO KWA WAZEE WA KOLANDOTO SHINYANGA,"SASA HAKUNA KUCHIMBA DAWA VICHAKANI"

Mmoja wa wazee wanaolelewa katika kituo cha Kolandoto katika manispaa ya Shinyanga

Choo kilichojengwa na kampuni ya Easyflex Production ya Shinyanga mjini kwa ajili ya wazee wanaolelewa katika kituo cha Kolandoto katika manispaa ya Shinyanga

Mkurugenzi wa  EASY FLEX PRODUCTION Bi. Happiness Kihama akiwa eneo la choo hicho

Meya wa manispaa ya Shinyanga Gulam Hafeez Mukadam akizungumza baada ya kuzindua choo hicho

Maneno yanayosomeka katika choo hicho

Hawa ni baadhi ya wazee wanaolelewa katika kituo cha Kolandoto Shinyanga

Haya ni magodoro 60 yaliyokabidhiwa na Easyflex Production kwa wazee wa Kolandoto,ikiwa ni msaada ulitolewa na Mgodi wa dhahabu wa Buzwagi uliopo Kahama unaomikiwa na kampuni ya uchimbaji madini ya ACACIA ambao waliahidi kuwasaidia wazee hao wakati wa harambee iliyoendeshwa na Easyflex Production mwaka jana
  Baadhi ya wazee wanaolelewa katika kituo cha Kolandoto





Baada ya wazee wanaoishi katika kituo cha makazi ya wazee wasiojiweza cha Kolandoto manispaa ya Shinyanga kulalamika kwa muda mrefu kutokana na tatizo sugu la ukosefu wa choo na kulazimika kutembea umbali mrefu kutafuta huduma hiyo vichakani hatimaye tatizo hilo limepatiwa ufumbuzi kwa kujengewa choo na Kampuni ya Uzalishaji na usambazaji wa Video na sauti EASY FLEX PRUDUCTION ya mjini Shinyanga.

Akitoa taarifa ya mradi wa ujenzi wa choo hicho na kukabidhi msaada wa viti 30 na magodoro 60 kwa ajili ya malazi ya wazee hao vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 20 mkurugenzi wa  EASY FLEX PRODUCTION Bi. Happyness Kihama amesema kampuni yake imeamua kuwajengea choo na kutoa msaada huo kutokana na kuguswa na matatizo yanayowakabili wazee hao kituoni hapo ikiwa pia ni kuwaepusha na magonjwa ya mlipuko kutokana na kujisaidia hovyo.


Kihama amesema msaada wote uliotolewa  unathamani ya sh 21.7 milioni ikiwa ni michango ya wadau mbalimbali, iliyotolewa kupitia harambee ambayo iliratibiwa na asasi hiyo katika kusaidia kambi ya wazee  na kituo cha watoto wenye ulemavu jumuisha cha Buhangija.

“Bado kuna changamoto kubwa katika kuielimisha jamii umuhimu wa kusaidia wenye mahitaji maalumu ,nawaomba wananchi na watanzania wenzangu tubadilike tusaidie makundi haya kwani hayana msaada mwingine zaidi yetu sisi wanajamii na tusiiachie serikali pekee haiwezi kutekeleza kila jambo “amesema Kihama.


Akipokea msaada huo na jengo la choo chenye matundu manne kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga Bw. Ally Rufunga mstahiki meya wa manispaa ya shinyanga Bw. Gullam Hafidh Mukadam pamoja na kuishukuru taasisi hiyo ameitaka jamii ya watanzania kuwa na mwamko wa kuanza kuwasaidia wazee na watu wenye mahitaji maalum badala ya kusubiri misaada kutoka kwa wahisani wa nje ya nchi hali ambayo imekuwa ikidhalilisha utu wa mtanzania. 


Kwa upande wao mlezi msaidizi wa kituo hicho Evodia Ndaka  na mwenyekiti wa makazi hayo Simon Maganga  wameiomba serikali kuzifanyia ukarabati mkubwa nyumba za makazi hayo ya wazee kutokana na majengo yake kuchakaa hali inayowafanya waishi kwa wasiwasi mkubwa na kwamba wamekuwa  wakilazimika kuzihama wakati wa mvua inaponyesha kutokana na kuvuja huku nyingi kati ya hizo tayari sehemu za kuta zake zimebomoka.

Hivi sasa kuna wazee  45 na watoto 16 wanaoishi katika kambi ya wazee wakoma ya Kolandoto manispaa ya Shinyanga 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527