Picha 30!! TIGO NA HMT WATOA MSAADA WA MADAWATI 600 KWA SHULE 8 ZA MSINGI SHINYANGAKutokana na changamoto ya uhaba wa madawati  katika shule za msingi mkoani Shinyanga,Leo kampuni ya simu za mkononi Tigo kwa kushirikiana na asasi iyosokuwa ya kiserikali ya Hassan Maajar Trust (HMT) wametoa msaada wa madawati 600 yenye thamni ya shilingi milioni 100  kwa  ajili ya shule  nane  za msingi mkoani humo.

Hafla fupi ya kukabidhi madawati hayo  yatakayotumika kwa wanafuzni 1800,imefanyika katika shule ya msingi Bugoyi A mjini Shinyanga ambapo mgeni rasmi alikuwa Katibu tawala mkoa wa Shinyanga Projestus Rutabanzibwa kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga.

Hafla hiyo imehudhuriwa pia na mkurugenzi wa kampuni ya Tigo kanda ya ziwa Ally  Maswanya na makamu mwenyekiti wa asasi isiyokuwa ya kiserikali ya Hassan Maajar Trust (HMT) Shariff Hassan Maajar.Wengine waliohudhuria hafla hiyo ni Wenyeviti wa kamati za shule,wakurugenzi wa halmashauri,maafisa elimu,walimu,wanafunzi,wadau wa elimu na watu mbalimbali wenye mapenzi mema.

Miongoni mwa shule 8 zilizopatiwa msaada huo ni Bugoyi A  madawati 80,Bugoyi B madawati  50,Msufini  70 shule zote za  manispaa ya  Shinyanga, katika halmashauri ya Shinyanga vijijini ni shule ya  Mwakitolyo  na Lyabukande ambazo zitapata madawati 80 kila moja na shule ya Busungo na Mwakuhenga zilizopo katika halmashauri ya Msalala kila moja itapata madawati 75.

Malunde1 blog ilikuwepo katika eneo la tukio,Mwandishi mkuu wa blog hii, Kadama Malunde ametuletea picha 30 za tukio zima........
Wa kwanza kushoto ni diwani wa kata ya Ndembezi palipofanyika hafla hiyo ambaye pia ni naibu meya wa manispaa ya Shinyanga David Nkulila ,akifuatiwa na mkurugenzi wa kampuni ya Tigo kanda ya ziwa Ally  Maswanya,katikati ni katibu tawala mkoa wa Shinyanga Projestus Rutabanzibwa(mgeni rasmi) akifuatiwa na makamu mwenyekiti wa asasi isiyokuwa ya kiserikali ya Hassan Maajar Trust (HMT) bwana Shariff Hassan Maajar

Makamu mwenyekiti wa asasi isiyokuwa ya kiserikali ya Hassan Maajar Trust (HMT) Shariff Hassan Maajar akizungumza wakati wa kukabidhi madawati hayo ambapo alisema ndoto ya  asasi  ya Hassan Maajar Trust (HMT) ni kuboresha  mazingira ya kusomea nchini Tanzania na kwamba wanachotaka ni dawati kwa kila mwanafunzi.
Wageni mbalimbali wakifuatilia kilichokuwa kinajiri katika viwanja vya shule ya msingi Bugoyi A mjini Shinyanga

Makamu mwenyekiti wa asasi isiyokuwa ya kiserikali ya Hassan Maajar Trust (HMT) Shariff Hassan Maajar alisema wanashirikiana na Tigo katika shughuli mbalimbali mfano baada ya kutoa msaada wa madawati mkoani Njombe sasa wametoa msaada mkoani Shinyanga.
Mkurugenzi wa kampuni ya Tigo kanda ya ziwa Ally  Maswanya akizungumza wakati wa hafla hiyo ambapo alisema msaada huo wa madawati 600 ni kidhibitisho cha jinsi ambavyo kampuni inajitolea kusaidia jamii kupitia kitengo chake cha uwajibikaji kwa jamii(CSR)

Mkurugenzi wa kampuni ya Tigo kanda ya ziwa Ally  Maswanya alisema msaada huo ni sehemu ya uwekezaji wa kampuni ya Tigo katika miradi ya kijamii yenye kuleta mafanikio makubwa katika maisha ya wanajamii na kwamba kupitia msaada huo Tigo inachangia katika kuboresha mazingira ya kusomea katika shule za Tanzania hivyo kuandaa madaktari,viongozi,wahandisi na wataalamu wengine wajao katika nyanja mbalimbali.

Wanafunzi wa shule ya msingi Bugoyi A wakiimba kwaya wakishukuru kupata msaada wa madawati

Wanafunzi wa shule ya msingi Bugoyi A wakiimba kwaya

Wanafunzi wa shule ya msingi Bugoyi A na B wakiwa eneo la tukio

Wageni mbalimbali wakiwa eneo la tukio

Waandishi wa habari nao walikuwepo

Mwalimu wa zamu bi Leticia Lima akiwa eneo la tukio na wanafunzi wake wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea
Mgeni rasmi Katibu tawala mkoa wa Shinyanga Projestus Rutabanzibwa kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga akizungumza wakati wa hafla hiyo ambapo alishukuru kwa msaada huo huku akiwataka wadau wengine kujitokeza na kusaidia katika harakati za kumaliza tatizo la madawati mkoani Shinyanga.


“Msaada huu unalenga kuondoa changamoto ya uhaba wa madawati katika shule zetu,tunaomba ushirikiano kwa wadau wengine kwani serikali pekee haiwezi kumaliza changamoto zilizopo katika shule hizi”,aliongeza Rutabanzibwa.


Tunafuatilia kinachoendelea


Wanafunzi wa shule ya msingi Bugoyi A wakiwa katika madawati yao 80 kabla ya kukabidhiwa rasmi leo

Kushoto ni mkurugenzi wa kampuni ya Tigo kanda ya ziwa Ally  Maswanya  na makamu mwenyekiti wa asasi isiyokuwa ya kiserikali ya Hassan Maajar Trust (HMT) Shariff Hassan Maajar wakiwa mbele ya madawati kabla ya kukabidhi
Wanafunzi wakiwa kwenye baadhi ya madawati hayo
Mgeni rasmi katibu tawala mkoa wa Shinyanga Projestus Rutabanzibwa kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga akijiandaa kukata utepe wakati wa zoezi la kukabidhi madawati hayo 600

Mgeni rasmi katibu tawala mkoa wa Shinyanga Projestus Rutabanzibwa baada ya kukata utepe ishara ya kukabidhi madawati 600

 
Eneo la makabidhiano
Shamra shamra zikiendelea

Kushoto ni mkurugenzi wa kampuni ya Tigo kanda ya ziwa Ally  Maswanya  na makamu mwenyekiti wa asasi isiyokuwa ya kiserikali ya Hassan Maajar Trust (HMT) Shariff Hassan Maajar wakifurahia jambo baada ya kukabidhi madawati hayo
Picha ya pamoja na mgeni rasmi

Hafla inaendelea
Hafla inaendelea katika viwanja vya shule ya msingi Bugoyi A
Walimu wakiwa eneo la tukio
Wanafunzi wakifurahia baada ya zoezi la kukabidhi madawati kumalizika

Wanafunzi wakiendelea kuchekelea

Furaha ilitawala
Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post