Hatari Sana!! JAMAA AGONGWA NA TRENI AKIVUKA RELI HUKO MOROGORO!!


Mtu mmoja  amefariki dunia baada ya kugongwa vibaya  na  treni wakati akivuka reli na kisha viungo vyake kusambaa  katika mtaa wa  ujenzi  Manispaa ya Morogoro .

Mashuhuda wa tukio hilo wamesema marehemu alijulikana kwa jina moja  la Mangi ambapo  wameeleza  kusikitishwa na ajali kwa kuwa  hii ni mara ya  tatu watu kugongwa na treni  katika maeneo hayo na kueleza kuwa   amarehemu alikuwa  anavuka  reli.
Naye mwenyekiti wa mtaa wa ujenzi Christopher Charles ameelezea  tukio hilo na kuwataka wananchi kuacha tabia ya kupita kwenye njia ya Reli kwani wataendelea kusababisha ajali  zisizo za lazima  ambazo zingeweza kuepukika. 
Askari wa jeshi la polisi wamefika katika eneo la tukio  na  kuchukua mwili wa marehemu ambapo umehifadhiwa katika  chumba cha maiti katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro.
Via>>ITV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post