Basi mtu wako nikakutana na bonge la HEADLINE mtandaoni yaani.. “10 of the Coolest Homes in the World“, nikaingia faster nijionee PICHA za hizo nyumba kali huko DUNIANI.
Nilizokutana nazo kiukweli ilibidi nicheke,alafu nikaona sio vibaya na wewe mtu wanguvu uzione labda iko itakayokuvutia na wewe ukatamani siku moja uwe nayo.
Ilinipa tabu kujua nini kinaendelea hapa. Naona kama mapango mapango tu hivi, lakini ndiyo mjengo huo mtu wangu. Bubble House, iko Ufaransa.
Mjengo huu uko Ivory Coast, hivi kama kuna watu mjusi tu wanaogopa, itakuwa kulala kwenye huyu mamba? Nyumba hiyo, inaitwa Crocodile House.
Buti la kijeshi??? Hapana, huo ni mjengo kabisa mtu kajitengenezea hapo, inaitwaShoe House, iko South Africa.
Hii ya Korea Kusini nayo iko kwenye list, inaitwa Toilet House, kwa juu ukiicheki ni kama choo kweli.
Social Plugin