Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Angalia Picha!! WATU 19 WAFARIKI KWA AJALI YA HIACE KUTUMBUKIA MTONI HUKO MBEYA,WALIKUWA 21!!


Watu 19 wamekufa na wengine wanne  wamejeruhiwa baada ya gari aina ya Hiace kuanguka katik eneo linaloitwa Uwanja wa Ndege , Kiwira Mkoani Mbeya.
 
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya, Bwana Ahmed  Msangi amesema watu 18 wamekufa papo hapo na mmoja amefariki dunia akiwa njiani  wakati akipelekwa Hospitali ya Misheni ya Igogwe kwa matibabu.
 
Kamanda MSANGI amesema kulikuwemo abiria 21 kwenye Hiace hiyo na miongoni mwa waliokufa ni dereva wa gari hiyo na ameongeza majeruhi aliozungumza nao wamemweleza walimtaka dereva apunguze mwendo,lakini hakupunguza mwendo.
 
Amesema kutokana na mgomo wa mabasi makubwa Mkoani Mbeya dereva huyo alitumia nafasi hiyo kubeba abiria hao ambao walikuwa wanakwenda mnadani.
 
Kamanda wa polisi mkoa wa mbeya amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema kuwa chanzo chake ni mwendo kasi, huku akiwata madereva kuwa makini barabarani ili kuepuka ajali zinazoweza kuepukika.
 
Hiace ikiwa mtoni


Hiace ikiwa mtoni
Wasamaria wema wakisaidiana na polisi kubeba miili ya majeruhi na waliopoteza maisha
Habari zaidi zitawajia punde tutakapozipata

Copy and WIN : http://ow.ly/KNICZ
Habari zaidi zitawajia punde tutakapozipata

Copy and WIN : http://ow.ly/KNICZ

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com