Ajali Hii ya Ajabu kweli!! WATU SABA WAFARIKI ,SABABU KUBWA NI KIBURI CHA DEREVA!!

Kano-Collapse
Hii picha ya ajali nimeiona kwenye baadhi ya mitandao ya Nigeria, imenishtua nikaona niifatilie ajali imetokeaje.


Ajali imetokea Kano, Nigeria ambapo watu saba wamefariki dunia na polisi wanafanya uchunguzi wa tukio hilo.

Habari kutoka eneo la tukio zinasema kuwa ajali hiyo imetokana na kuanguka kwa daraja la waenda kwa miguu lilil0kuwa likiendelea kujengwa katika barabara.

“Mafundi waliokuwa wanajenga waliwakataza watu wasipite na magari chini ya daraja kwa sababu bado kazi ya ujenzi ilikuwa ikiendelea, huyo dereva wa taxi alikiuka agizo hilo..
 alikuwa anakatisha na gari ikiwa na abiria, daraja likaanguka.. wamefariki watu saba..“– Magaji Majiya, msemaji wa Jeshi la Polisi.
d3
Daraja ambalo lilikuwa likijengwa lilikuwa kama hili.

Mara nyingi ujenzi ukiwa unaendelea kwenye barabara kunakuwa na vibao vya maelekezo lakini watu wengi huwa hawazingatii maelekezo, ndicho ambacho kimetokea kwenye hii ajali ya Nigeria.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post