Michepuko Noma!! JAMAA ANG'ATWA SEHEMU ZAKE ZA SIRI AKIMLAZIMISHA SHEMEJI YAKE WAVUNJE AMRI YA 6!!


Maria Ionita akiwa na mumewe, Florin Ionita hospitalini.
MWANAUME aitwaye Florin Ionita, 53, ameng'atwa sehemu yake nyeti na rafiki wa mkewe wakati akijaribu kumlazimisha afanye naye mapenzi.

Wauguzi waliokuwa wakimpatia huduma Florin Ionita.
Florin Ionita na mkewe Maria Ionita, 49, walikuwa katika karamu huko Chisinau nchini Moldova wakiwa na rafiki wa mkewe.
Baada ya karamu hiyo, Maria aliamua kuwapeleka baadhi ya marafiki zake nyumbani kwao huku nyuma akimuacha mumewe akiwa na rafiki yake mwenye umri wa miaka 24.

Florin Ionita akiendelea kupatiwa huduma baada ya kung'atwa nyeti zake.
Cha kushangaza baada ya dakika 30, Maria alirudi eneo la karamu kumfuata mumewe na kukuta akilia kwa maumivu na kumwambia: "Niitie gari la kubeba wagonjwa, sehemu yangu nyeti itadondoka"
Kufuatia tukio hilo, Maria alitaka kujua kilichotokea ndipo rafiki yake akamweleza kuwa mumewe alimlazimisha afanye naye mapenzi na kuvua suruali ndipo akaamua kujihami kwa kumng'ata sehemu zake nyeti.
Maria aliamua kumsamehe mumewe kwa kusema: "Nimemsamehe maana alikuwa akijaribu kufanya kitendo ambacho wanaume wengi hutaka kukifanya, ila nilipowapigia watu wa gari la kubeba wagonjwa sikufanya haraka, na niliwaambia wasifanye haraka sana kufika eneo hilo"
Mwanamke huyo mbali na kuwaambia wasifanye haraka watu wa gari la kubeba wagonjwa, pia aliwatajia eneo ambalo si husika ili kumpa fundisho mumewe huyu mchepukaji.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527