Kali kutoka Shinyanga!!! AHUKUMIWA JELA MIAKA 20 KWA KOSA LA KUMUOA DADA YAKE ALBINO,WAZAZI WABAKI MIDOMO WAZI!!


Mahakama ya wilaya ya kahama mkoani Shinyanga Juzi imemuhukumu kwenda jela miaka 20 Ally Sanyiwa (24) kwa kosa la kumuoa dada yake Mektilda Sanyiwa(20) mkazi wa Chela.

Imedaiwa mahakamani hapo na mwendesha mashitaka wa polisi Koplo Evodia mbele ya hakimu mfawidhi George Mariki kuwa mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo mwezi machi mwaka huu.

Aidha koplo Evodia ameiambia mahakama hiyo kuwa mtuhumiwa huyo aliweza kumtorosha dada yake na kisha kumpeleka katika kijiji cha Mazimba na kuishi naye.

Wazazi wa Mektida ambaye ni mlemavu wa ngozi (albino) wamesema kuwa mara baada ya binti yao kutoweka nyumbani walipata hofu na kuanza kumtafuta mpaka alipopatikana akiwa anaishi nyumba moja na kijana wao.

Mahakama hiyo imetoa hukumu kwa mtuhumiwa huyo mara baada ya kukiri kutenda kosa hilo ambalo ni kinyume na maadili ya kitanzania.
via>>Farajimfinanga.com

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527