Jingine Jipya!! BARAZA LA KILIMO LAPINGA ACT KUTUMIKA KAMA JINA LA CHAMA



Baraza la Kilimo Tanzania (ACT) limekitaka chama cha siasa cha ACT – Tanzania kutotumia jina hilo kwa kuwa tayari baraza hilo limekwsha sajili jina la ACT kama kifupi cha jina la Baraza hilo.

Akizungumza leo katika kipindi cha Hotmix cha EATV kinachoruka kila Jumatatu hadi Ijumaa saa 12:00 hadi saa 2:00 jioni, Mwenyekiti wa Baraza hilo Dkt Sinare Yusuf Sinare amesema kuwa jina ACT linatambulika kama kifupi cha Agricultural Council of Tanzania na kwa mujibu wa taratibu za hati miliki, jina hilo (ACT) halitakiwi kutumika na watu wengine hata kama litaambatanishwa na maneno mengine.

“Hata kama wakiongeza maneno, bado kuna ACT, hiyo ni nembo yetu, tumekwisha andika barua kwenda kwa msajili wa vyama vya siasa, pia tumeandika barua kwenda katika chama hicho lakini bado hatujapata majibu, nimekwisha ongea na Zitto Kabwe kuhusu hilo na kumweleza kuwa wanatakiwa kurekebisha kabla hatujaenda hatua za juu zaidi(Mahakamani) ambazo ni ghali.” Amesema Dkt Sinare.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527