NOTI BANDIA NA SARE ZA JWTZ ZAMPONZA ASKARI MAGEREZA HUYU,ATIMULIWA KAZI BILA HURUMA HUKO SIMIYU,YULE ASKARI WA FFU NAYE KWISHA HABARI YAKE!!


Edmund Masaga ambaye alikuwa askari magereza katika gereza la wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu, ambaye jana amefukuzwa kazi kwa kile kilichodaiwa kukutwa na noti Bandia.




Naibu kamishna wa jeshi la polisi Mkoani Simiyu Charles Mkumbo akiwaonyesha waandishi wa habari (hawapo pichani) baadhi ya fedha bandia ambazo zilikamatwa askari wa jeshi la polisi Mkoani Simiyu pamoja na Askari Magereza wilayani Bariadi


Jeshi la Magereza nchini limemfukuza kazi askari wake wa Gereza laBariadi, Mkoani Simiyu kwa kosa la kupatikana na fedha za bandia kinyume na sheria za cchi.

Kwa mujibu wa taarifa rasmi iliyotolewa jana na Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, John Casmir Minja, askari Na. B. 6499 Wdr. Edmund Masaga amefukuzwa kazi kwa fedheha kuanzia Machi 28, 2015 kwa kosa la kulidhalilisha Jeshi mbele ya Umma kinyume na Kanuni 22(xlix) ya Kanuni za Utumishi wa Jeshi la Magereza za Mwaka 1997.

Aidha, Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, John Casmir Minja amekemea vikali vitendo hivyo kwani ni kinyume cha Maadili na Utendaji ndani ya Jeshi la Magereza huku akiwataka askari wote wa Jeshi la Magereza nchini kutenda kazi zao kwa uadilifu na uaminifu mkubwa.

Hata hivyo taarifa kutoka katika jeshi la polisi Mkoani Simiyu zinaleleza kuwa Tayari askari wake mwenye namba H 2420 PC Seleman Juma (25) ambaye ni askari wa kikosi cha kutuliza gasia FFU Mkoani Simiyu Tayari amefukuzwa kazi na Ijumaa wiki iliyopita wote wawili walifikishwa mahakamani.  

Chanzo>> http://simiyunews.blogspot.com

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527