PICHA- IGP MANGU AONGOZA MAZISHI YA POLISI ALIYEUAWA KWA KUKATWA MAPANGA AKIOKOA MTOTO HUKO DODOMA,MTUHUMIWA AUAWA PIA
Thursday, February 05, 2015
Inspekta
Jenerali wa Polisi (IGP) Ernest Mangu akiongoza leo waombolezaji katika
kutoa heshima za mwisho kwa Askari Namba G. 7168 PC JOSEPH ISACK SWAI
aliyeuwawa huko Chango’ombe ya juu Mkoani Dodoma na mtu aliyefamika kwa
jina la TISSI SIRIL MALYA.
Wasifu wa marehemu ukisomwa
Maombolezo wakati wa shughuli ya kuaga mwili wa askari huyo shujaa
Na Sylvester Onesmo wa Jeshi la Polisi Dodoma.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kama Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi
DAVID MISIME – SACP amesema kama alivyotoa taarifa jana tarehe
04/02/2015 kuhusiana na kuawa kwa Askari Namba G. 7168 PC JOSEPH ISACK
SWAI huko Chango’ombe ya juu Mkoani Dodoma na mtu aliyefahamika kwa jina
la TISSI S/O SIRIL MALYA.
Jeshi la
Polisi Mkoa wa Dododoma lilianza msako wa kumtafuta mtuhumiwa huyo baada
ya kufanya kitendo hicho cha kinyama cha kumkata kata kwa panga
kichwani na mikononi Askari huyo.
Kamanda
MISIME amesema majira ya saa 23:00hrs usiku wananchi walimuona maeneo ya
Mti Mkavu Mailimbili Mkoani Dodoma akiwa bado na lile panga alilotumia
kumuua Askari.
Hata
hivyo walichukua sheria mkononi na kumshambulia sehemu mbalimbali za
mwili wake, Polisi walifika eneo la tukio na kumchukua kisha kumkimbiza
Hospitali ya Mkoa lakini daktari akagundua ameshafariki.
Aidha
Kamanda MISIME amesema mtuhumiwa huyo katika kumbukumbu walizonazo ni
kwamba mwaka 2006 aliwahi kufungwa miaka mitatu (3) kwa kosa la
kujeruhi, Pia mwaka 2009 alifungwa tena miezi sita (6) kwa kosa la
kutishia kuua.
Ametoa
pongezi kwa wananchi kwa kuonyesha kuchukizwa na kitendo alichomtendea
Askari hyuo lakini waache kujichukulia sheria mkononi.
Pia
ametoa wito kwa wananchi tuanze kuchukua hatua kurekebisha maadili
kuanzia ngazi ya familia kwani tumeelezwa kuwa mtuhumiwa alikuwa ni
mvutaji bangi kiasi kwamba ilimfanya awe anafanya vitendo ambavyo ni
kinyume na maadili na sheria za nchi.
Askari Joseph Swai enzi za uhai wake
Askari Joseph Swai enzi za uhai wake
Mwili wa askari Joseph Swai baada ya kuuawa
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com
🚧🚦 Usiendeshe gari lako bila Mafunzo na Leseni halali_ 📲 Wasiliana nasi sasa: wa.me/255740273285 Unahitaji nini? 🚘 Unataka kujifunza udereva wa magari na kupata Cheti? 📄 Una cheti unataka kupata Leseni? 🔄 Unajua kuendesha lakini huna cheti wala leseni na unataka refresh upate cheti? 🛣️ Una nyaraka zote muhimu lakini unahitaji kujifua zaidi barabarani? ✅ Una Leseni bila cheti na unataka renew? 🌍 Tupo mikoa yote Tanzania hadi vijijini! 📞 Tupigie sasa: 0769 763 285
Social Plugin