Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro Leonard Paulo amesema jeshi la
polisi lilifika katika eneo la tukio na kufanikiwa kuwakamata watu watatu
wanasadikiwa kujihusisha na tukio hilo na linaendelea kuwahoji kisha
watafikishwa mahakamani.
Aidha kamanda Paulo amesema jeshi la polisi linaendelea kumtafuta
mtuhumiwa aliye kimbia ambapo katika hatua nyingine wamefanikiwa
kumkamata hawara wa mtu huyo aliyejulikana kwa majina ya Husuna Isimaeli
mkazi wa mkindo ambaye alikuwa akimhifadhi mtuhumiwa na jeshi la
polisi litaendelea kumshikilia kwa mahojiano ilikumpata mtuhumiwa aliye
kimbia.
Social Plugin