HIZI HAPA AINA ZA VYAKULA UNAVYOHITAJI ILI KUPUNGUZA UZITO

051613-251842-cook-the-book-sardines-in-spicy-tomato-sauce


Moja kati ya matatizo yanayowakumba watu wengi kwa kizazi cha sasa ni tatizo la uzito , tatuizo hili limekuwa chanzo cha matatizo mengine makubwa na yenye madhara makubwa kwa afya ambayo wakati mwingine husababisha kifo .

Magonjwa ya moyo , kisukari , shinikio la damu la kupanda na kushuka , nguvu za kiume , matatizo ya figo na viungo vingine vya mwili pamoja na kukosa mvuto wa kawaida yanasabishwa na mtu kuwa na uzito ambao anashindwa kuumudu .

Uzito huongezeka kutokana na mtindo Fulani wa maisha ya mwanadamu na pia unaweza kupungua kutokana na mtindo huu huu wa maisha ambao kama ukimudu kuuzingatia hasa kwenye chakula unaweza kupungua uzito na kuishi maisha kwa raha na kwa afya salama .

Ifuatayo ni orodha ya vyakula vya aina nne tofauti ambavyo unaweza kuanza kuvipanga kwenye chakula chako ambavyo visaidia sana kupungua uzito .

1.Mayai Mazima
Katika miaka ya hivi karibuni tafiti nyingi ambazo si sahihi na si za kweli zimesababisha watu kutozingatia ulaji wa mayai hasa yakiwa mazima na muhimu kuliko yote ni ile sehemu ya kiini cha yai . 

Watu wengi wameaminishwa kuwa kiini cha yai kina mafuta ambayo ulaji wake huweza kufanya mtu anenepe bila mpangilio.
Mafuta yanayopatikana kwenye kiini cha yai si mafuta mabaya bali ni yale amabyo mwili inayahitaji na hayana hatari kwa mwili wa binadamu .
Whole-eggs-sl
Kiini cha yai kina virutubisho muhimu sana kwa mwili wa mwanadamu ikiwemo protini pamoja na chembechembe zinazosaidia kupunguza sumu mwilini .

2.Chokoleti Nyeusi .
Tafiti nyingine zisizo sahihi zimewaaminisha wengi kuwa chokoleti sio kitu kizuri , lakini ni kinyume chake kwani si kila chokoleti zina madhara kwa mwanadamu na baadhi yake ikiwemo zile nyeusi zina faida kubwa mwilini .
The-Benefits-of-Dark-Chocolate-for-Valentine’s-Day-Recipe-Included
Asilimia 70 ya chembechembe zinazotengeneza chokoleti nyeusi ni kokoa , chokoleti hii ina virutubisho pamoja na madini muhimu mwilini kama vile Magnesium  pamoja na manganese ambayo husaidia mwili katika masuala mbalimbali ikwiemo kuponya vidonda na kuridishia chembechembe hai za mwili zinazopotea .

Chokoleti nyeusi pia husaidia kupunguza uwezekano wa mtu kupata maradhi ya moyo na maradhi mengine yatokanyo na shinikizo la damu .

051613-251842-cook-the-book-sardines-in-spicy-tomato-sauce
3.Samaki Wadogo ‘Dagaa’.
Samaki wadogo ambao hufahamika kama dagaa wana faida nyingi sana mwilini , sababu kubwa ya faida yao ni jinsi amabvyo wanaliwa wazima kwa maana ya ngozi yao , mifupa na vitu vyote vilivyomo ndani yake ambavyo kimsing vina faida kubwa sana .
Dagaa wana kila kitu ambacho mwili wa mwanadamu unahitaji kwa maana ya virutubisho ambavyo vinaboresha afya na kumpa mtu nguvu pamoja na kinga dhidi ya magonjwa na pia kusaidia kuponya magonjwa pale mtu anapokuwa mgonjwa .

  1. Nyama ya Ini .
Katika hali ya kawaida ile kauli ya kusema kuwa nyama nyekundu si nzuri kwa mwanadamu ina usahihi wake na ina mahali ambako si sahihi .

Usahihi wake ni kwamba , nyama nyekundu si nzuri kwa mwili wa mwanadamu . Lakini kuishia hapo ndio mahali ambako kauli hii inacha kuwa sahihi , kwani ukweli ni si nyama zote nyekundu si nzuri kwa mwanadamu kuna nyama ambazo ni sahihi na nyingine si sahihi . 

Nyama ya ng’ombe na mbuzi zina madhara makubwa zinapoliwa kwa wingi na pasipo mpangilio .
2006-11-01-urban-bachelor-cooking-pork-liver
Lakini kuna nyama nyekundu ambazo zinahitajika mwilini na mojawapo kati ya nyama hizi ni nyama ya ini .

Hata wanyama kwa mfano simba wanafahamu hili na ndio maana Simba anapoua mnyama huanza kula viungo vyake vy andani kabla ya kula sehemu nyingine .

Nyama ya ini virutbisho muhimu kama vile Vitami A , madini mbalimbali kama Shaba , Zinc , Selenium , Folate na Niacin pamoja na Protini kwa kiwango kikubwa sana . 

Virutubisho vyote hivi vina faida kubwa sana mwilini mwa mwanadamu . Kula nyama ya ini hata mara moja kwa wiki ina faida kubwa sana .

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post