Moja kati ya vyakula vinavyomletea mlaji wake harufu kali ni vitunguu swaumu ambavyo huumika kama viungo kwenye chakula .
Vitunguu swaumu vina vitu Fulani ndani yake amvayo hujitokeza pale
kinapokatwa , kusagwa au hata kutafunwa vitu hivi kitaalamu hufahamika
kama Allicin na Allin na hivi ndio hasa husababisha harufu kali ambayo
hutokea baada ya mtu kula vitunguu swaumu au vyakula vilivyoungwa
kutumia vitunguu swaumu .
Pamoja na hayo vitunguu swaumu vina faida kubwa sana mwili mwa
mwanadamu na faida hizo huletwa na hii Illin ambayo inatajwa kuwa sababu
ya harufu yake mbaya na moja kati ya faida zake ni jinsi ambavyo
vitunguu swaumu husaidia kupambana na bacteria wanaoleta magonnjwa
mbalimbali na virusi tofauti .
Mbegu ya Binzari
Mbegu ya Binzari hutumika kwenye mapishi ambapo huleta ladha nzuri
kwenye chakula , hata hivo mbegu hizi husababisha harufu mbaya ambayo
inabakia mdomoni kwa muda mrefu . Kama unataka kupunguza harufu mbaya
unaweza kuipunguza kwa kunywa maji mengi na kutumia vyakula vingine
ambavyo vinatumika kupunguza harufu ambavyo havina harufu kali .
Nyama nyekundu ni moja kati ya vcyakula vinavyosababisha harufu mbaya
mdomoni na tumboni . Ni vigumu kwa wtau wengi kukubaliana na hili kwa
kua nyama nyekundu ni moja kati ya vyakula vinavyopendwa sana na watu .
Tafiti zinaonyesha kuwa jasho jingi ambalo husababishwa na mafuta
yanayoganda mwilini kutokana na ulaji wa nyama nyekundu ni moja kati ya
vitu ambavyo huleta harufu mbaya kwenye mwili wa mwanadamu .
Nyama nyekundu ni moja kati ya vyakula sugu kwa kusababisha harufu mbaya mdomoni na inayotokea tumboni .
Kama unataka kupunguza harufu kutokana na nyama nyekundu ni vyema
ukapunguza na kuanza kula nyama itokanayo na samaki na wanyama wengine
wa baharini .
Mboga Za Majani
Baadhi ya mboga za majani zinasababisha harufu mbaya mwilini nazo ni cauliflower , kabichi, broccoli na nyinginezo nyingi .
Kahawa
Kahawa nayo iko kwenye orodha ya vyakula ambavyo vinasababisha harufu
mbaya mdomoni na mwilini kwa jumla . Moja vitu ambavyo vimo ndani ya
kahawa ambavyo ni Caffeine husisimua mfumo wa neva yaani ile mishipa ya
fahamu mwilini na husababisha mtu avuje jasho kwa wingi kuliko kawaida .
Social Plugin