![]() |
| Madiwani wakifuatilia kikao cha kupitisha bajeti ya mwaka 2015/2016 |
![]() |
| Kikao kinaendelea |
![]() |
| Kikao kinaendelea |
![]() |
| Madiwani wakifuatilia kinachoendelea ukumbini |
![]() |
| Kikao kinaendelea |
![]() |
| Waandishi wa habari wakiwa ukumbini |
Halmashauri ya manispaa ya
shinyanga imepitisha mapendekezo ya mpango
wa bajeti zaidi ya shilingi
bilioni 36 kwa
kipindi cha mwaka 2015/2016 kwa
ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.
Mapendekezo hayo yamepitishwa
leo na baraza la madiwani katika kikao maalum cha bajeti kilichofanyika kwenye
ukumbi wa mikutano wa mkuu wa mkoa wa Shinyanga.
Akiwasilisha mapendekezo ya bajeti hiyo katika baraza la madiwani
mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga Festo Kang’ombe amesema katika mwaka wa fedha 2015/2016 lengo la
manispaa ni kukusanya Shilingi bilioni 36.
Amesema kati ya pesa hizo
shilingi bilioni 2.5 zitakusanywa katika mapato yake ya ndani halmashauri,ruzuku
kutoka serikalini bilioni 24 na ruzuku kutoka nje ya nchi shilingi zaidi ya
shilingi bilioni tisa.
Kang’ombe amefafanua kuwa
katika kipindi cha mwaka 2015/2016 Halmashauri hiyo inatarajia kukusanya zaidi ya shilingi bilioni mbili kutoka katika
vyanzo vyake vya ndani kiasi ambacho ni sawa na ongezeko la asilimia kumi na
nne ikilinganishwa na makisio ya shilingi bilioni mbili na milioni mbili katika
mwaka wa fedha 2014/2015.
Aidha mkurugenzi huyo amesema
sehemu kubwa ya ongezeko la mapato hayo ya ndani yanatarajiwa kukusanywa kutokana na kodi za ardhi,ada ya viwanja,ushuru wa
mazao,ada ya minada, pamoja na leseni za biashara.
Na Kadama Malunde-Shinyanga.








Social Plugin