ANGALIA PICHA- MAJANGA YA SHINYANGA MJINI WIKI HII

Baada ya Tanesco kuacha tabia ya kukata umeme hovyo hovyo tena bila taarifa,japokuwa wanakata  na kurudisha ingawa siyo sana,sasa wakazi wa manispaa ya Shinyanga wanakabiliwa na tatizo la maji kukatwa bila taarifa ambapo tunaambiwa kuwa mamlaka ya maji Safi na  usafi wa  Mazingira katika manispaa ya Shinyanga SHUWASA imekata maji katika maeneo mbalimbali mjini Shinyanga tena bila taarifa,leo siku ya 7.Unaambiwa dumu moja la maji la lita 20 linauzwa shilingi 1000 ukihurumiwa sana unauziwa shilingi 800,hutaki nenda kachote kwenye visima vya watu binafsi au ishi bila maji.

v
Foleni katika moja ya visima virefu nyumbani kwa mtu

Hekaheka za maji mtaani

Tunasubiri maji

SHUWASA hatuna hamu nao!!Anafuata maji auze mtaani,safari yake moja shilingi 8000/=
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post