ANGALIA PICHA- GWIJI PATRICK KLUIVERT AFUNGUA KITUO CHA MICHEZO KOM SEKONDARI MJINI SHINYANGA

Patrick Kluivert na Wanamichezo wa KOM Sekondari katika picha ya pamoja
Hapa ni katika Shule ya Sekondari KOM ya Mjini Shinyanga ambako jana jioni Mchezaji gwiji na nyota wa zamani wa Ajax Amstadam, Barcelona ya Hispania na NewCastle ya Uingereza Patrick Kluivert  ambaye hivi sasa ni kocha msaidizi wa timu ya taifa ya Uholanzi alifungua kituo cha Michezo katika shule hiyo kilichopewa jina la "Patrick Kluivert Academy Sport Club". 

Patrick Kluivert alikuwa ameambatana na mbunge wa Shinyanga mjini mheshimiwa Stephen Masele ambaye pia ni Naibu Waziri wa nchi Ofisi ya Makamo wa Rais anayesimamia Muungano na Mazingira( Ameletwa na mbunge huyo).Lengo la kufunguliwa kwa kituo hicho cha Michezo ambacho kitakuwa na aina zote za michezo ikiwemo Gym kitakachokuwa kinatumiwa na wanafunzi wa shule hiyo na maeneo mengine ya jirani
picha zote na Kadama Malunde-Shinyanga

Awali mkurugenzi wa Shule ya Kom sekondari Jackton Koyi akimkaribisha Patrick Kluivert katika shule yake kwa ajili ya kufungua jengo la michezo katika shule hiyo


Kushoto ni mbunge wa Shinyanga mjini Stephen Masele akizungumza katika shule ya Sekondari KOM ambapo
alisema lengo la kufungua kituo hicho ni kuinuna vipaji vya watoto wenye uwezo wa kucheza mpira kwani siku zote kipaji huonekana kwa mtu akiwa bado mdogo.
Masele alisema Jengo hilo litakuwa na vifaa vyote vya michezo ikiwemo Gym na kuwatakia kila la heri wale wote watakaopata nafasi ya kutumia kituo hicho.Wa kwanza kulia ni Patrick Kluivert
 
 Patrick Kluivert akizungumza jambo na mbunge wa Shinyanga mjini Stephen Masele
 
 Muda mfupi baada ya kuwasili katika shule ya Kom Sekondari,mheshimiwa Stephen Masele(wa tatu kutoka kushoto) akiwa na mgeni wake Patrick Kluivert( wa pili kushoto),mkurugenzi Kom Sekondari Jackton Koyi( wa kwanza kushoto) na mwalimu wa michezo KOM Sekondari Michel Odelo( wa kwanza kulia) wakielekea kwenye jengo la michezo katika shule hiyo jana jioni
Mwalimu KOM Sekondari akiongoza msafara kuelekea kwenye jengo la Michezo kwa ajili ya ufunguzi wa kituo cha Michezo katika shule hiyo
Mkurugenzi wa KOM Sekondari Jackton Koyi akitoa maelekezo kwa wageni wake
Msafara kuelekea kwenye jengo la michezo katika shule ya sekondari Kom kwa ajili ya ufunguzi
Baada ya kufungua kituo hicho cha michezo,hapa ni mbele ya jengo hilo Mheshimiwa Masele akipiga makofi na wadau wengine wa michezo
Baada ya ufunguzi Patrick

Picha ya pamoja Patrick Kluivert na walimu wa Kom Sekondari,wa pili kutoka kulia ni mkuu wa wilaya ya Kishapu Wilson Nkhambaku,wa kwanza kulia ni
Mwalimu wa michezo KOM Sekondari Michel Odelo alisema wamefurahishwa na ujio wa Kluert na kwamba ujio wake utakuwa chachu ya kuinua vipaji vya wachezaji wa mpira na kuwaomba wazazi kupeleka wenye vipaji vya kucheza mpira katika kituo hicho ili kutengeneza wachezaji wazuri wa baadaye watakaousaidia mkoa wa Shinyanga na Taifa kwa ujumla katika michezo.


Wakuu wa wilaya za Shinyanga na Kishapu nao walikuwepo,wa kwanza kushoto ni Wilson Nkhambaku wa Kishapu akifuatiwa na Annarose Nyamubi wa Shinyanga


Picha za kumbukumbu zikaendelea kupigwa hapo Kom sekondari
Patrick Kluivert na Wanamichezo wa KOM Sekondari

Mkurugenzi wa KOM Sekondari Jackton Koyi akiwa na Patrick Kluivert-picha zote na Kadama Malunde-Shinyanga
BOFYA HAPA UONE PATRICK KLUIVERT ALIPOKUTANA NA STAND UNITED UWANJA WA KAMBARAGE SHINYANGA 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post