ANGALIA PICHA 16- MAZISHI YA MSANII MEZ B MKOANI DODOMA

PBF_4318 
Mez B alifariki Ijumaa ya February 21 2015 nyumbani kwao Dodoma baada ya kulazwa hospitali Dodoma zaidi ya mara nne toka mwishoni mwa mwaka 2014, tatizo kubwa lilikua ni kifua na mgongo ambapo Jumatatu ya February 23 2015 ambapo Mamia ya mashabiki na wasanii wa muziki wa kizazi kipya,walijitokeza kuupumzisha mwili wa msanii, Moses Bushangama ‘Mez B’, katika makaburi ya Wahanga wa Treni, Maili mbili mkoani Dodoma.


Mpaka anafariki Mez B hakuwa ameoa wala hana mtoto ambapo pia amefariki siku chache kabla ya kuachia single yake mpya kwenye Radio na TV

 
Akizungumza wakati wa kuuaga mwili huo, mama wa marehemu, Mchungaji Mary Katambi, aliwataka vijana kumrudia Mungu. 
 
“Mwanangu aliuona uwepo wa Mungu, nilikuwa nikimsihi kuokoka na kumrudia Mungu na alikuwa akinijibu itafika wakati mimi wa yeye kufanya hivyo,” alisema Mary.
 
 Upande wake msanii wa kundi la Chemba Squad, Noorah alisema wamesikitika kumpoteza Mez B kwani alikuwa ni msanii anayependa ushirikiano na pengo lake halitaweza kuzibika.
IMG-20150223-WA0040
Wananchi wakiwa wamebeba  mwili wa marehemu Marehemu Mez B baada ya kuagwa na mashabiki wa mziki pamoja na ndugu jamaa na marafiki mwili wake ulielekea kupumzishwa katika makaburi ya Wahanga Maili mbili jana.
IMG-20150223-WA0036
Mama mzazi wa Mez B, Marry Mkandawile (katikati) akiwa ameshikiliwa na ndugu baada ya kuingia viwanja vya Mashujaa ili kutoa heshima za mwisho.
IMG-20150223-WA0037 IMG-20150223-WA0038
Baadhi ya wasanii waliohudhuria msiba wa Mez B wakiwa kwenye majonzi mazito
IMG-20150223-WA0039  IMG-20150223-WA0041 IMG-20150223-WA0042 IMG-20150223-WA0044
Mtangazi wa Citizen TV anayejulikana kwa jina la Mzazi Willy Tuva akifanya mahojiano na msanii wa Bongo Fleva Janjaro.
~mpekuzihuru

PBF_4313Baadhi ya Wasanii waliojitokeza kumzika ni pamoja na Dogo Janja na Raymond wa Tiptop Connection, Hemedy PHD, Gelly wa Rymes, Baba Levo, M2theP, Noorah na Dark Master kutoka Chemba Squad.
PBF_4294 PBF_4289
PBF_4192
PBF_4252
PBF_4549

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post