UMOJA wa Kutetea katiba ya
Wananchi UKAWA umesema utasusia zoezi la upigaji wa kura wa Katiba
iliyopendekezwa na Bunge Maalum la katiba inayotarajiwa kupigwa mwezi wa
nne mwaka huu kwa Madai Rais Jakaya Kikwete amekiuka makubaliano na
Vyama vya siasa waliokubaliana mwaka jana mjini Dodoma.
Azimio hilo limetangazwa leo Jijini Dar Es Salaam
na Mwenyekiti mwenza wa Umoja wa vyama Vikuu vya Upinzani
vinavyounda Umoja wa kutetea Katiba ya Wananchi UKAWA Freeman Mbowe,
wakati wa mkutano na Waandishi wa habari ambapo amesema Umoja huo
hauwezi kuwepo katika mipango ya kuingamiza nchi wakati wa kupitisha
katiba isiyokuwa na chembe yeyote ya kumsaidia mtanzania.
“Tunasema
kwa pamoja hatutoshiriki katika katika kura za wa kupitisha katiba ya Chama Cha Mapinduzi,katiba iliyotengenezwa bila ya kuwa na maridhiano ya
Kisiasa,maana Rais Kikwete ameamua kwa maksudi kabisa kutusaliti sisi
viongozi wenzake wa kisiasa,tulikubaliana kwamba Bunge lile lisitishwe
kutokana na kutoweza kupatikana kwa katiba mpya lakini alivyotoka pale
akatusaliti na kuendelea na Bunge lile lilotafuna pesa za wananchi walalahoi”alisema mbowe.
Mbowe aliongeza kuwa katika makubaliano hayo walifikia maazimio ya
kufanyia mabadiliko katiba iliyopo ya mwaka 1977 katika vipengele
mbalimbali ikiwemo kipengele cha kuwepo tume huru ya uchaguzi lakini
Rais Kikwete akawageuka dakika za mwisho.
Mbowe ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Hai alizidi kusema kwa uchungu kwamba
Umoja huo umebaini rafu mbalimbali wananazozifanya Chama cha mapinduzi
ili katiba iliyopendekezwa iwe katiba harala kwa kuwasafirisha watu
kutoka Mkoa wa dare s Salaam hadi Visiwani Unguja na pemba ili wakati wa
kupiga kura ya kupitisha katika Iliopendekwa na bunge waipigie kura ya ndio ambapo Mbowe anasema wao hawatakubali.
Kwa upande wake mwenyekiti wa chama cha NLD Dk. Emmanuel
Makaidi amesema chama chake kitazunguka nchi nzima kuhamasisha wananchi
kutopigia kura katiba pendekezwa kwa Madai Katiba hiyo ina mapungufu
kibao na itazidi kuwaweka katika mazingira magumu yenye kujaa umasikini.
Naye Mwenyekiti wa chama cha NCCR Mageuzi James Mbatia alisema
anashangaa kitendo cha Rais Kikwete kuwageuka na kuyatupia mbali
makubaliano yao waliosema mchakato usitishwe mpaka baada ya uchaguzi
mkuu na kufanyia marekebisho ya Katiba iliyopo na kusema kitendo hicho
kinaonyesha kiongozi huyo alivyokuwa kigeugeu na umoja huo hautokubali.
Vilevile Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF Profesa Ibrahimu Lipumba
alisema Katiba wanayoitaka kuipitisha kinguvu haina mshiko kwa
watanzania na imekaa kwa ajili ya kuwanafaisha watawala walioko
madarakani,na akasema chama chake hakitokubali kuwepo katika dhambi ya
kuwahujumu wa Tanzania na wao watasusia mchakato huo.
Vyama Vinavyounda UKAWA ni CUF,Chadema,NCCR mageuzi na NLD
Na Karoli Vinsent-Dar es salaam