Hii Kali !! BABA MWENYE NYUMBA AMBURUZA MAHAKAMANI MPANGAJI WAKE KISA KAHARIBU SAKAFU KWA MKOJO!!!


Mahakama moja nchini Ujerumani imempa idhini mwanamume mmoja kujisaidia haja ndogo akiwa amesimama baada ya mwenye nyumba kutaka alipwe akidai kuwa sakafu ya bafu lake iliharibiwa na mkojo wa mpangaji wake. 
 Mpangaji amekataa kumlipa mmiliki wa nyumba akisema ni haki yake kusimama akiwa anaenda haja ndogo

Mwenye nyumba ambaye alitaka kulipwa dola 2,200 kwa uharibifu uliofanyika, alidai kwamba sakafu yake iliyotengenezwa kwa mawe aina ya Marble iliharibiwa na mkojo.

Lakini jaji aliamua kwamba njia aliyotumia mwanamume huyo kujisaidia inaambatana na tamaduni nyingi ,akisema kuwa mtu anapojisaidia akiwa amesimama ni jambo la kaiwada sana.

Kuna mjadala nchini Ujerumani kuhusu ikiwa wanaume wanapaswa kujisaidia haja ndogo wakiwa wanasimama au wakiwa wamekaa kwenye choo.

Baadhi ya vyoo nchini Ujerumani haviwaruhusu watu kujisaidia wakiwa wamesimama, lakini wale wanaoamua kuketi chini huitwa "Sitzpinkler", ikimaanisha kwamba wao sio kama wanaume na sio jambo la kawaida kwa wanaume kukaa wakiwa wanajisaidia haja ndogo.

Jaji Stefan Hank alikubaliana na ripoti ya wataalamu kwamba tindikali inayotokana na mkojo au Euric Acid, huharibu sakafu nyingi za vyoo.

Lakini kwa kukamilisha amri yake, jaji alisema kwamba wanaume wanaosisitiza kusimama wanapojisaidia haja ndogo, mara kwa mara huvurugana na wenye nyumba lakini hawawezi kuamrishwa kulipa ikiwa sakafu itaharibika. 
 Via>>BBC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post