MWENYEKITI WA KIJIJI WA CCM ANUSURIKA KUPIGWA KWENYE MKUTANO WA HADHARA

 http://www.itv.co.tz/media/image/KIPIGO.jpg

Wananchi wa kijiji cha Puma katika wilaya ya Ikungi mkoani Singida wamemkataa mwenyekiti  wa kijiji hicho katika mkutano wake wa kwanza na kusababisha diwani wa kata hiyo  kwa kushirikiana na jeshi la polisi kuingilia kati na kufunga mkutano kabla ya wakati ili kumnusuru asipigwe na wananchi.

Wananchi hao waliokuwa na hasira wamesema hakuna sababu ya kuwa na mwenyekiti ambaye wananchi hawamkubali kwa sababu katika uchaguzi uliopita kulikuwa na udanganyifu katika upigaji kura.
Kutokana na hali hiyo wamesema ni bora kuachana na vyama vya siasa wachague mwenye kiti wa kimila ili kukisaidia kijiji cha Puma kupata maendeleo.
Baada ya vurugu  kuongezeka diwani wa kata hiyo kwa tiketi ya CCM,Bwana Ramadhani Kulungu ilibidi kufunga kikao hicho ili kuweza kumnusuru mwenyekiti wa kijiji cha Puma na kuwatuliza wananchi ili kusitokee uvunjifu wa amani.
Mwenyekiti wa kijiji cha Puma  kwa tiketi ya CCM ,Bwana Sifa Joramu awali ambaye alishindwa kabisa kuendesha kikao chake ,baada ya jeshi la polisi kuingilia kati na kuamua kumsindikiza kwa ulinzi mkali huku wananchi wakimzomea na kusema hawamtaki,amesema hizo ni fujo za vyama vya upinzani lakini yeye  atahakikisha kazi anafanya kwa sababu yeye ndiye aliyeshinda na kuapishwa kwa kazi ya uwenyekiti wa kijiji cha Puma. 
Kundi la watu waliamua kumfuata na kumbeba  juu kisha kumzungusha mitaani Bwana Hassan Chaimbo aliyegombea kwa tiketi ya CHADEMA na kushindwa kwa kupata kura mianne arobaini na nne dhidi ya  Bwana Sifa  Joramu alishinda uenyekiti wa kijiji cha Puma kwa tiketi ya CCM katika uchaguzi uliofanyika mwishoni  mwaka jana na kupata kura mianne hamsini na saba.
via>>ITV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post