Mwanamke aitwaye Maria Haule mkazi wa Kijiji cha Muhukuru Songea vijijini mkoani Ruvuma ameuawa kwa kukatwa na shoka
kichwani na mume wake aitwaye Salvatory Ndimbo na kisha mwili wake
kuutupa mto Mkurumo.
Kamanda wa polisi wa mkoa wa Ruvuma ACP Mihayo
Msikhela anasema chanzo cha mauaji hayo ni ugomvi wa
kimapenzi ambapo marehemu Maria Haule mwenye miaka arobaini alikuwa na
uhusiano wa kimapenzi na mwanaume mwingine aitwaye Anzekula na kutaka
kuachana na mumewe Salvatory Ndimbo mwenye miaka sitini.
Jeshi la polisi linaendelea kumsaka mume wa marehemu Maria Bw. Ndimbo mbaye ametoroka baada ya kufanya unyama huo.