Leo Katoro Geita Hapatoshi!! WATANGAZAJI WA RADIO FREE AFRICA KUVAANA NA WADAU WA SALAMU KATIKA MECHI KABAMBE


Kikosi cha Timu ya Mpira wa Miguu cha Radio Free Africa kutoka Sahara Media Group Ltd leo Jumamosi ,saa kumi jioni kinatarajia kushuka katika uwanja wa CCM Katoro katika mechi kabambe itakayowakutanisha na timu ya watuma salamu wa Katoro mkoani Geita.

Nahodha wa timu ya RFA Bernard James (Cheza Kidansi) amesema watangazaji wa Radio Free Africa wamejipanga vizuri kuhakikisha wanapata ushindi wa kishindo katika mechi hiyo.

James ameongeza kuwa malengo ya mchezo huu kwanza ni kukutana na wadau wa radio free africa ikiwa ni pamoja kujenga urafiki na kufahamiana kati ya watangazaji na wasikilizaji (wadau)

Amesema baada ya mchezo huo kikosi cha timu ya Radio Free Africa kinajipanga  kuwavaa wadau wa igunga tabora na baadaye kufuatiwa na wadau wa babati manyara.

Akitoa majina ya kikosi kinachokwenda kufanya mauaji hayo leo mkoani geita james amesema ni pamoja na:

1.William Bundala (Kijukuu cha bibi k)

2.Renatus Kiluvia (Bizzo)

3.Jackson Nyamsuka

4.Bernard James (Captain)

5.Dady James

6.Yusuph Magasha.

7.Godfrey Kusolwa

8.David Azaria.

9.Emmanuel Mkuwi

10.Wambura Mtani(Cotinho)

11.Juma Baragaza.

James ameongeza kuwa wachezaji wasaidizi ni pamoja na,

1.Dj John Lyatuu.
2.Dalton Mgala.
3.Salehe Masesa.
4.Elia Migongo.
5.Steve Moyo Mchongi.

Mchezo huo utakuwa na kiingilio cha shilingi 2000/= tu getini.
 Hii si ya kukosa mwanawane!!!!


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527